Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka mfereji wakati alipokagua
mradi wa mashamba ya umwagiliaji ya vitunguu katika kijiji cha Mang’ola
Barazani Wilayani Karatu wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Arusha akihimiza na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM
ambayo hata hivyo katika wilaya ya Karatu imeonekana kukwamishwa na
Mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Israel Natse
Chadema, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na madiwani kwa kuitenga baadhi
ya miradi ambayo ipo katika vijiji ambavyo madiwani na wenyeviti wa vijiji wanatoka Chama cha Mapinduzi CCM ambapo wananchi wa kijiji hicho wamemlalamikia Kinana.
Mfano
mradi wa Kituo cha afya cha Baray Mbuga Nyekundu ambapo serikali kuu
ilitenga na kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 60 katika
halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kituo hicho, lakini
fedha hizo zimeondolewa katika mradi huo na madiwani hao na hazijulikani
zimefanya kazi gani huku wananchi wakitaabika kwa kutopata huduma nzuri
za afya kijijini hapo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-KARATU-ARUSHA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kufukua mchanga kwenye mfereji unaopitisha maji kwa ajili ya kumwagilia
mashamba ya vitunguu katika kijiji cha Mang’ola Barazani wilayani
Karatu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda vitunguu pamoja na wananchi katika mashamba hayo.
Baadhi
ya wananchi wakiwa wamekaa juu ya mti wakati walipokuwa wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani alipozungumza
nao kwenye mkutano wa hadhara kijijini Mang’ola.
Baadhi
ya wananchi wakiwa wamekaa juu ya mti wakati walipokuwa wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani alipozungumza
nao kwenye mkutano wa hadhara kijijini Mang’ola.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kjiji cha Mang’ola.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumwaga zege katika ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Rhotia wilayani Karatu.
Mbunge
wa viti maalum Kupitia vijana CCM mkoa wa Arusha Catherine Magige
akiwasalimia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara
mjini Karatu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na kujibu
hoja mbalimbali ambapo aliwaambia maswali mengi yanaelekea kwa mbunge wa
jimbo hilo, madiwani na mwenyekiti wa halmashauri kwa kuwa ndiyo wenye
kusimamia miradi na kuwapa taarifa wananchi, Lakini viongozi hao
wamekuwa wakifanya mambo wanavyotaka na kuacha wananchi wakipata taabu.
Hata
hivyo Kinana amesema wananchi wa Karatu ni watanzania na wana haki ya
kupata huduma mbalimbali za maendeleo na serikali ya CCM haitawaacha
kama wanavyoachwa na viongozi wao wa CHADEMA waliowachagua wenyewe.
Mmoja wa vijana waliohama CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapunduzi CCM akizungumza na wananchi katika mkutano huo.