Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) katikati akiingia katika viwanja vya Salender Bridge Club wmara
baada ya kumalizika kwa matembezi ya amani yaliyolenga kuhamasisha umma
kuhusu kujali afya zao jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kulia ni Rais wa Chama Cha
Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro.
Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na
wananchi wakishiriki matembezi ya amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) na wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania
(TDA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno
iliyofanyika katika viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es
Salaam. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya hiari yalioyoanzia
katika viwanja hivyo na kupitia Barabara ya Diomond Jubilee kabla ya
kurudi uwanjani hapo kupitia barabara ya AlhasanMwinyi na Kauli mbiu ya
wiki ya Afya ya Kinywa ni “Tabasamu la Maisha” Katikati ni Rais wa Chama
Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro na
wa mwisho kulia ni Rais Mteule wa Chama hicho Dkt. Ambege Mwakatobe.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) akipeana mkono na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno
Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro (kulia) jana jijini Dar es Salaam
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno.
Baadhi
ya Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na
baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya
Afya ya Kinywa na Meno wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla
hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) akiangalia baadhi ya machapisho yanayohusu Afya ya Kinywa na Meno
kwenye banda lililowekwa katika Viwanja vya Salender Bridge Club jana
jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa
Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kushoto ni Rais wa Chama Cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(MB) (wapili kutoka kushoto) akiwa katika matembezi ya amani ikiwa ni
katika hfla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini
Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini/WHVUM.