WAZIRI MIGIRO AKABIDHI NAKALA ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA WALEMAVU, TAASISI ZA KIDNI NA ASASI ZA KIRAIA

March 16, 2015

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Watanzania wametakiwa kuisoma katiba inayopendekezwa kwa umakini ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika kuandika historia mpya ya nchi.

Hayo aliyasema leo Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Asha-Rose Migiro wakati akikabidhi katiba inayopendekezwa kwa makundi mbalimbali,Migiro amesema nchi itaandika historia mpya baada ya kupata katiba mpya.

Alisema wananchi wakisoma katiba kwa umakini kutasaidia kufikia matarajio katika kutengeneza ramani ya nchi kwa kuvuka miaka 50 ya katiba mpya.

Migiro amesema kuwa wamechapisha katiba inayopendekezwa kwa watu wenye ulemavu wa kuona kwa alama ya nukta nundu na baada ya kupita kwa katiba watapewa kwani ni haki yao kuwa nayo.

“Kujitokeza kwenu ni ishara ya kuunga mkono kwa katiba inayopendekezwa hivyo ni wajibu wenu kutoa elimu ili waweze kufanya maamuzi wakati wa kupiga kura ya maoni”amesema Dk.Asha-Rose.

Aidha wamechapisha nakala hizo kwa herufi kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili nao waweze kusoma na kuelewa na kuweza kufanya maamuzi.

Migiro amesema wamechapisha nakala na kugawa kwa nchi nzima ambapo kila kata inapata nakala 300 na Zanzibar zinagaiwa chini ya ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

Baadhi ya wadau waliopokea nakala hizo wamesema watafikisha,lakini hawawezi kuwaamulia katika maamuzi yao
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015). Dkt. Turuka alipokea kwa niaba ya Makatibu Wakuu wenzake.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa mwakilishi wa Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam Sheikh Mussa Kundecha katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia) katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akimkabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa mwakilishi wa Taasisi ya Mabohora Bw. Zainuddin Adamjee katika hafla fupi ya kugawa nakala hizo kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za kidini katika hafla fupi ya kugawa nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Machi 16, 2015).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu wake Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia katika hafla fupi ya kugawa nakala za Katiba Inayopendekezwa zilizoandaliwa na Serikali kwa taasisi mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana (Jumatatu, Machi 16, 2015). (Picha: Farida Khalfan, Wizara ya Katiba na Sheria)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »