TAMISEMI YATOA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA WAPYA

March 16, 2015

Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia akizungumza mapema leo katika siku ya kwanza ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba yanayoendelea katika ukumbi wa hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu) Bw. Zuberi Samataba.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne A. Sagini akitoa mada kuhusu kazi na majukumu ya Wakuu wa Wilaya katika semina hiyo iliyoanza leo tarehe 16 hadi 19 Machi 2015.
Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute Profesa Joseph Semboja, ambaye pia ndiye mwezeshaji mkuu wa mafunzo hayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma. UONGOZI Institute ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais inayoshughulikia mafunzo kwa viongozi waandamizi serikalini pamoja na kufanya utafiti na ushauri wa sera kwa serikali.
Mshiriki wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Shaban Kissu akichangia mada wakati wa mafunzo. Mada moja wapo zilizojadiliwa leo ni kuhusu mahusiano na mawasiliano baina ya serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda akizungumzia kuhusu changamoto mbali mbali za Wakuu wa Wilaya. Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na maadili na sheria za kazi.
Baadhi ya wahudhuriaji wa kundi la Wakuu wa Wilaya wapya ishirini na saba wakifuatilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mafunzo ya Wakuu wa Wilaya Wapya yanayoendelea mjini Dodoma.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »