WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA MFUMO WA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA VITUO VYA AFYA TANZANIA BARA

September 11, 2015


 Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kulia), akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa taarifa ya vituo vya afya nchini uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa   wizara hiyo, Hermes Rulagirwa na Ofisa wa Tehama, Kenani Mwansasu.
 Hapa ni kupongezana baada ya uzinduzi huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa   wizara hiyo, Hermes Rulagirwa (kulia), akizungumza na wanahabari.
 Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
  Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya wakati wa uzinduzi huo.
………………………………..
Na Dotto Mwaibale
 
SERIKALI imezindua mfumo mpya wa kuhifadhi  taarifa za vituo vya huduma ya afya vya Serikali na binafsi katika ngazi ya kanda, mtaaa kijiji na mkoa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua mfumo huo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando alisema kupitia mfumo huo watumiaji watapata taarifa za vituo sahihi na namna vinavyotoa huduma.
Alisema mfumo huo utatumik kama chanzo pekee cha taarifa za vituo na mwisho utumiwe na wananchi kupata taarifa za huduma zinazotolewa na kituo husika.
“Mpango huu wa kielektroniki wa kuandaa mipango na kufanya maamuzi madhubuti wa sekta ya afya nchini, tunaomba na tunahitaji sana kushirikiana katika kuboresha huduma za afya na kuwatendea haki Watanzania,” alisema.
Aliongeza kuwa utatengeneza namba maalum kwa kila kituo kitakachoingizwa na namba hiyo haitarudiwa hata kama kituo hicho kitafungwa.
Dk.Mmbando aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali kwa kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini na kuwaaagiza waganga kuhakikisha wanafanya update kila wakati ili kuendana na wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha  Tehama Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Hermes Rulagirwa alisema kupitia mfumo huo utatawawezesha kujua sehemu ya kituo kilipo na huduma wanazozitoa.
Alisema kabla ya kuzinduliwa kwa mfumo huo wapo waganga kutoka vituo mbalimbali nchini walipatiwa mafunzo.
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »