…………………………
Na matukiodaima Blog
MGOMBEA
Ubunge wa jimbo la Iringa kupitia chama cha mapinduzi ( CCM) Frederick
Mwakalebela amesema jimbo la Iringa Mjini limekosa kunufaika na fursa za
maendeleo kwa kuwa halikuwa na mbunge makini wa kuleta maendeleo .
Hivyo
amewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuecha kujutia kukosa
maendeleo na badala yake kumchagua kuwa mbunge wao ifikapo Octoba 25
mwaka huu.
Mwakalebela
ametoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano wake wa kampeni za Ubunge
kwenye kata ya Mshindo alisema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo
hilo atahakikisha anasogeza maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Jimbo la
Iringa ambao kwa miaka mitano wamekosa kupata maendeleo hayo .
Kwani
alisema hakuna sababu ya kujutia na badala yake kutumia nafasi hiyo
kujutia miaka mitano ambayo wamepumzika pasipo kushuhudia maendeleo
yoyote katika jimbo hilo la Iringa mjini.
Kuhusu
nini atafanya baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge alisema ni pamoja na
kuboresha miundo mbinu ,kuanzisha saccos ya vijana ,kuanzisha mfuko wa
elimu wa jimbo kwa kutumia sehemu ya mshahara wake ,kuwawezesha wazee
kupata matibabu ya bure na kuboresha sekta ya michezo.
Wakati
aliyekuwa Mgombea Ubunge katika mchakato wa kura za maoni Balozi
Augustino Mahiga alisema matumaini mapya ya jimbo la Iringa yatapatikana
kwa kuchagua diwani ,mbunge na Rais toka CCM .
Kwani
alisema kuwa majuto ya wanajimbo la Iringa ambayo wanayo kwa sasa ni
kutokana na kukosa mbunge Makini wa kuwatumikia wananchi na badala yake
kuwa na mbunge wa maandamano na fujo bungeni.
|