PRESS CLUB ZANZIBAR YAFANYA UCHAGUZI NA KUSISITIZA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

August 10, 2015
unnamed (73)
Katibu Mkuu msaafu wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Suzan Peter Kundambi katikati akitoa taarifa ya mwaka kwa Wanachama wa Jumuiya hiyo katika mkutano wa Mwaka wa ZPC ulioambatana na uchaguzi. Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (74)
Wajumbe walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (75)
Wajumbe walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (76)
Katibu Mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akiomba kura kwa Wanachama (hawapo pichani)kabla ya kufanyika Uchaguzi huo. Katibu huyo anashika nafasi ya Suzan Peter mara baada ya kushika nafasi hiyo katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo uliambatana na uchaguzi huko ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
unnamed (77)
Mweyekiti mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) kulia akipongezana na aliyekuwa mpinzani wake katika nafasi ya Uenyekiti Suleiman Abdallah mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
………………………………………………………………………………..
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 
WAANDISHI wa habari nchini wamesisitizwa kulinda maadili ya kazi zao ikiwemo kutumia kalamu zao vizuri hasa kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa ikiwa waandishi watatumia vibaya kalamu zao basi wanaweza kuvuruga hali ya amani na utulivu na kuweka nchi katika hali ya machafuko.
Hayo yalielezwa na Meneja Bima ya Maisha Tawi la Zanzibar Aisha Rubenic Makorogo, wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari uliombatana na Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya uliofanyika katika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Alisema, kazi muhimu ya wanahabari ni kuona wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na kutokubali kutumiwa vibaya na watu wenye maslahi binafsina badala yake wafanye majukumu yao kwa kutenda haki kwa pande zote ili nchi iweze kuvuka salama.
Aidha alisema, tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika jamii ambayo inategemewa na kila mtu kwani inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanachi wanaoishi mijini na vijijini kupata habari zinazotokea nchini kupitia vyombo wanavyofanyia kazi.
Meneja huyo, aliwaomba waandishi kufanya kazi kwa ueledi wa juu ili kuona nchi yao inaendelea kuwa na hali ya utulivu na usalama.
Hata hivyo, aliwaomba wanachama wa ZPC kuchagua viongozi ambao wataweza kuiimarisha na kufanya Jumuiya yao iondokane na utegegemezi wa misaada huku wakiwa wabunifu ambao watachagua njia mbadala itakayowaletea kipato katika jumuiya yao.
“Ili kuweza kufanikiwa na jumuiya yenu kuimarika zaidi basi ni vyema kujenga mshikamano na wanachama wenu na kuwa wabunifu wa kutegemea vyanzo vingi vya kujiingizia mapato ili kuikuza jumuiya yenu,” Aliwaasa Meneja Aisha.
Sambamba na hayo aliwaomba wanajumuiya hao kujiunga na Bima ya maisha ambayo inatoa fursa nyingi kwa malengo ya maisha ya baadae kwa mwanachama.
Nae Mjumbe mstaafu wa Kamati Tendaji wa Jumuiya hiyo Suleiman Seif Omar, akitoa shukrani kwa niaba ya wanajumuiya wenzake waliahidi kuendelea kudumisha maadili ya kazi zao na wajibu wao katika kuitumikia jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Viongozi wapya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Abdalla Abdul-rahman Mfaume aliwaomba wajumbe kuzidisha mashirikiano na kuwaahidi kufanya kazi kwa moyo mmoja ili kuiletea ZPC maendeleo na Taifa kwa ujumla.
Mkutano huo mkuu ulimchagua Abdalla Abdul-rahman Mfaume kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo baada ya kupata kura 40 na kumshinda mpinzani mwenzake Suleiman Abdalla ambae amepata kura tisa,
Katibu Mtendaji wa ZPC Faki Mjaka ambaye hakuwa na Mpinzani alipata kura 46 na Naibu Katibu Mwinyimvua Nzukwi alipata kura 37 baada ya kumshinda Takdir Ali aliyeata kura 13.
Makamo Mwenyekiti wa Jumiya hiyo ni Abdalla Pandu aliyepata kura 28 na kumshinda Rahma Suleiman aliyepata kura 23. Mshika fedha Halima Tamim Thuwein aliyekuwa Mgombea pekee alipata kura 49 .Wajumbe sita wa kamati tendaji ni Aziza Hassan, Ghania Mohammed, Mwashamba Haji Juma,  Ishaka Omar, Maulid Hassan Kipevu na Saleh Hassan.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »