Meneja
Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habri Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar
baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni
Mtangazaji, Dina Marios.
……………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
KITUO
cha Redio cha EFM kimeamua kuendelea kufanya tamasha la muziki Bar kwa
Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza.
Hayo
yalibainishwa na Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo hicho, Denis Ssebo
wakati akizungumza na waandishi wa habri Dar es Salaam leo asubuhi
kuhusu tamasha hilo.
“Baada
ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza,
na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena Kituo chetu cha Redio
cha Efm kimekubali ombi hilo na sasa tamasha hilo linarudi tena kwa
kishindo likiwa limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi
zaidi” alisema Ssebo.
Alisema
Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na
mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu
wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa
utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.
Ssebo
alitaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa Muziki mnene bar kwa
bar utakaoporomoshwa na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha,
Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kigamboni na maeneo mengine
mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Alisema
Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 5
mwaka huu lakini katika kuelekea huko efm imeanza na muziki mnene bango
katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka
bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye
zawadi kibao.
Aliongeza
kuwa mwishoni kutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika
jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo
vingi sana.
“Ninawaomba
wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia
Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao
cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm
ambayo kwetu Muziki unaongea”. alisema Ssebo.
Ssebo
alipenda kutumia fursa hiyo kuwajulisha umma kwamba katika kuhakikisha
wanaendelea kutoa burudani iliyobora zaidi kupitia vipindi vyao
mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo
mkubwa wame mtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo
wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake wenye uwezo mkubwa katika
familia ya Efm. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com simu namba 0712-727062)