Washiriki wa Manjano Dream-makers katika taasisi ya Manjano Foundation
wamehitimu mitihani yao ya mwisho ya jinsi ya kupaka vipodozi (makeup).
Kuanzia sasa, washiriki hao wanawake na wasichana 30 wanaianza safari
yao ya mwaka mzima katika kujikita na ujasiriamali. Taasisi ya Manjano
Foundation, ilianzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa programu ambayo
itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwezesha kujiongezea kipato na
ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha
yake.
Kundi
hili la washiriki waliohitimu mafunzo mbali mbali linabeba bendera
yake, Manjano Dream-Makers, ukiwa ni mradi unaokusudia kuzaa kizazi
kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch
Manjano.
Mradi
huu uliandikwa na kuandaliwa na kampuni ya SSC Consulting wakiwa ndio
washauri wakuu wa mradi huu, hasa katika kuandaa Utaratibu na mipango
yote ya mafunzo ya biashara na ujasiriamali. Mradi huu unadhaminiwa na
kampuni ya Shear illusions kwa lengo la kuwajengea uwezo wanwake wa
Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya LuvTouch Manjano
kujisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua
Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa
Kitanzania. Kila
mshiriki amepewa mtaji wa bidhaa za LuvTouch Manjano, vitendea kazi
kumuwezesha kuwapodoa wateja, mafunzo ya biashara na ujasiriamali na pia
atapewa Business Coach na Mentor (Dada mshauri) ili kumuongoza katika
safari hii ya mwaka mzima katika kujikita kwenye ujasiriamali.
Tunawatakia kila la kheri kizazi kipya hiki cha wajasiriamali kina mama.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Muasisi wa
Mradi aliouanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye
Ujasiriamali.Mafunzo Chini ya Taasisi ya Manjano Foundation.Lengo la
Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa
bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri
kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa
lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.