BREAKING NEWS : ACT WAZALENDO WAMCHUKULIA FOMU YA URAIS PROFESA MKUMBO

August 17, 2015

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA Cha ACT-Wazalendo wamechukua
fomu kwa ajili ya mgombea urais atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchukua fomu ya urais,Katibu Mkuu wa Chama hicho,Samson Mwigamba amesema kamati kuu imempitisha Profesa Kitila Mkumbo kuperusha bendera katika uchaguzi utaofanyika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu. Mwigamba amesema kuwa wamejipanga katika kushinda uchaguzi huo kutokana na watu waliokupwepo katika chama hicho
ni wazalendo wa vitendo.

Amesema kuwa watu amesema chama chao ni kidogo lakini wameweza kusimamisha wagombea wa,Udiwani,pamoja na ubunge
ambapo katika vyama vyote vilivyoanizisha kwa kipindi kifupi vilishindwa
kufanya hivyo.
Aidha amesema wanamuamini Profesa
Mkumbo kutokana na malengo ya uanzishaji wa chama hicho kwa kutoa mchango
mkubwa hivyo lengo la chama limetimia.
Amesema ambao wanahamia katika Chama
hicho watapimwa uadilifu wao katika kuweza kuwatumikia wananchi wanao wachagua
katika nafasi mbalimbali.
ACT-Wazalendo wamechukua fomu kwa
kuwa idadi ndogo kuliko vyama vyote na utulivu ulitawala katika ofisi za tume
ya Tifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwakilishi wa chama cha ACT WAZALENDO na Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akipewa maelekezo na Afisa tawala wandamizi wa Tume ya uchaguzi (NEC),George Baasha kuhusiana na vitu vinavyotakiwa kwenye uchaguzi mkuu pamoja na kampeni zitakazo anza hivi karibuni.
Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akimwakilisha Dkt. Kitika Mkumbo kupokea fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO amechukua fomu hizo leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akionyesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT WAZALENDO mara baada ya kupokea fomu hiyo katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa chama ACT WAZALENDO, Samsoni Mwigamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »