Sentensi 5 za Adebayor kuhusu kumfukuza kwake mama yake na kumtelekeza

November 21, 2014
Adebayor-and-mum
Mapema leo asubuhi ilitoka habari kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Togo kumfukuza mama yake kwenye moja ya nyumba zake huko nchini Togo kutokana na kutokuwa na maelewano na mazuri na mama yake huku zikitoka taarifa kwamba kisa cha yote haya ni tuhuma za uchawi.
Masaa kadhaa baada ya habari hiyo kusambaa kwenye mitandao, Emmanuel Adebayor amekanusha kumfukuza mama yake kwenye nyumba kwa sababu ya alidhani anampiga misumari.
Dada yake Adebayor Maggie alikaririwa kupitia radio ya Peace FM kwamba mshambuliaji huyo amegoma kumhudumia mama yake na hajaonana nae kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mama yake ameripotiwa kuuza mifuko, makufuri na bidhaa nyingine ili aweze kuisadia familia yao.
Hata hivyo mshambuliaji huyo anayelipwa £101,000 kwa wiki amekanusha madai hayo ya dada yake kwamba amemtelekeza mama yake.
Adebayor, nae kwa upande wake alitafutwa na Peace FM, alisema: ‘Sijawahi kumfukuza mama yangu kwenye nyumba yangu. Aliamua kuondoka mwenyewe.
‘Nawezaje kuwa na mawasiliano na mama yangu ikiwa yeye anamwambia kila mtu kwamba sitoendelea mbele kwenye kazi yangy, hivyo nimeamua kuwa mwenyewe nifanye mambo yangu.
‘Inabidi waache kuongea kuongea, na waache kunifanyia uchawi, waniache peke yangu.
‘Nimemnunulia nyumba ya $1.2m huyo mtu anayejiita dada yangu. Unaweza kuamini huyo dada alienda kuipangisha hiyo nyumba bila kunifahamisha? – Alimaliza Adebayor

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »