BLOG

SOMA TARUJA LEO

SOMA TARUJA LEO

TAWODE

TAWODE

Monday, November 20, 2017

NAIBU WAZIRI HASUNGA AKABIDHI MSAADA WA MABATI KWA SHULE YA MSINGI ILIYOATHIRIKA NA KIMBUNGA MKOANI IRINGA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakitwanga Kinu wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) jana Mkoani humo.

Na Hamza Temba - WMU
....................................................................
Katika jiihada za Serikali za kuendeleza ushirikiano na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi nchini, Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa msaada wa mabati sitini kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule ya msingi Kipanga baada ya kuezuliwa na kimbunga hivi karibuni katika kijiji cha Ubwachana Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.

Msaada huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga alipotembelea kituo cha Malikale cha Isimila mkoani humo ambacho kinapakana na shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Mkoani humo.

Akikabidhi mabati hayo, Naibu Waziri Hasunga alisema  Serikali inatambua mchango wa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kwenye uhifadhi shirikishi hivyo ni jukumu la Serikali kuwaunga mkono pale wanapopatwa na majanga ya aina mbalimbali.

Aidha, aliwataka baadhi ya wananchi wanaochimba mchanga kwenye maeneo ya vivutio katika kituo hicho waache mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwakuwa wanahatarisha uhai wa kingo za miamba ya kale ambayo na kivutio kikubwa cha utalii wa asili katika ukanda wa kusini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya mambo ya Kale wa Wizara hiyo, Bi. Digna Tillya alitoa rai kwa wananchi wanaozunguka kituo hicho kushirikiana na Serikali katika uhifadhi na ulinzi wa kituo hicho na kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa mazingira.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiwa amevaa “musk’ mfano wa vazi la kabila la wahehe wa Mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake katika Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa huo (Boma) jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubwachana, Donatus Lihoha mabati 60 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Kipanga ambayo iliezuliwa na kimbunga hivi karibuni ikiwa ni kutambua mchango wa wananchi katika uhifadhi shirikishi wa Kituo cha Mali Kale cha Isimila jana Mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na Uhuishaji, Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale wa Wizara hiyo Digna Tillya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha na Uhuishaji, Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini wakati akitoa maelezo kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa  (Boma) wakati wa ziara yake jana Mkoani humo. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia kwake).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na watumishi wa Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) alipotembelea Makumbusho hiyo jana wilayani Iringa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela kuhusu Makumbusho ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa (Boma) wakati wa ziara yake jana Mkoani humo. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wapili kushoto) akisalimiana na wafanyakazi wa  (Kituo cha Mali Kale cha Isimila) alipotembelea kituo hicho jana mkoani Iringa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akimpa maelekezo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya (kulia) alipotembelea Kituo cha Mali Kale cha Isimila mkoani Iringa jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Digna Tilya akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mabati.
Baadhi wa washiriki wa hafla hiyo.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.

CCM MKOANI MBEYA YAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA MHE MWANJELWA KUWA NAIBU WAZIRI WA KILIMONaibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na wajumbe wa kamati ya siasa mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017. Picha zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku mara baada ya kuwasili kuwasalimu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya akiwa ziarani Mkoani humo, Jana Novemba 20, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya

Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kimemshukuru na kumpongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua Mhe Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuhudumu katika nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya tano.

Pongezi hizo pamoja na shukrani zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa wakati akitoa taarifa ya chama hicho Ofisini kwake Mara baada ya Naibu Waziri kuzuru katika Ofisi hizo akiwa ziarani Mkoani Mbeya.

Nkambaku alisema kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi muhimu kwani Mhe Mwanjelwa ni mchapakazi na msaada mkubwa kwa chama hicho hivyo uteuzi huo umeonyesha Imani kwa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Mkoa mzima wa Mbeya.

Aidha alimsihi Kutenda haki na kufanya kazi kwa bidii huku CCM ikiahidi kutoa ushirikiano mwema Kwa Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Mbeya.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasihi makada hao Kutofanya kazi za Chama kwa Mazoea badala yake kufanya kazi kwa weledi ili kuwasaidia wanachama na wasiokuwa wanachama wa CCM katika shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri Huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) amejivunia malezi bora na muhimu aliyoyapata ndani ya Chama Cha Mapinduzi huku akiwasihi viongozi kuongeza bidii katika kumsaidia Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Tanzania Mpya kwa manufaa ya watanzania katika kuwaletea maendeleo.

MBUNGE MGAYA AWASAIDIA WANAWAKE VYEREHANI 370 NJOMBE

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Katikati Mstari wa Mbele) akiwa na baadhi ya wanawake aliowakabidhi vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 Halmashauri ya Makambako Mkoani Njombe ili wajikwamue kiuchumi.
 Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA (Mbele) akiwa na baadhi ya wanawake aliowakabidhi vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 Halmashauri ya Makambako Mkoani Njombe ili wajikwamue kiuchumi.
Baadhi ya vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 90 vilivyolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA vikiwa tayari kukabidhiwa kwa baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Njombe ili wajikwamue kiuchumi.

Na Mwandishi Wetu, Makambako Njombe

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe NEEMA MGAYA ametoa msaada wa vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya Milioni 90 kwa wanawake mkoani humo ili wajikwamue kiuchumi huku akiunga mkono juhudi za Serikali inayohimiza uchumi wa viwanda.

Akizungumza Mjini Makambako wakati wa hafla ya kukabidhi vyerehani hivyo kwa baadhi ya wanawake, MGAYA amesema amefikia uamuzi huo ili kuunga mkono juhudi za Rais DK John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa taifa la uchumi wa kati kupitia viwanda.

Akibainisha zaidi ameeleza juhudi za kumkomboa mwanamke wa mkoa wa Njombe ni jambo linalopiganiwa kwa miaka mingi hivyo vyerehani hivyo vitawafungulia njia kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Nimekuwa sina papara katika utendaji wangu, mwaka jana nilitoa msaada wa vitabu vya ziada kwa Shule za Sekondari Halmashauri ya Makambako, ambapo kwa mwaka huu nimeamua kuunga mkono juhudi za serikali upande wa viwanda kwa kuwasadia wanawake hawa vyerehani hivi 370,” alisema Mgaya.

Akifafanua amesema anatambua thamani kubwa walionayo wanawake hivyo kwa kuwawezesha vyerehani hivyo kutainua familia na jamii zinazowazunguka kwani fedha zitakazopatikana zitasaidia huduma za kijamii na mahitaji mengine.

“Mtu ninayemthamini huwa nampa kitu ambacho kitadumu na kumsaidia kwa muda mrefu, mimi nimeamua kutowapa samaki kwani mtamla ataisha, nimewapa nyavu ambayo mtaitumia kuvua samaki, nendeni mkavitunze vyerehani hivi kujiletea maendeleo endelevu,” alisema Mgaya.

Akizungumza baada ya kupokea cherehani yake Diwani wa Viti Maalum Lupembe Neema Limbanga amesema alilolifanya Mbunge huyo wa Viti Maalum halijawahi kutokea katika maisha yake na kwamba vyerehani hivyo vimewafungulia njia kimaisha.

Naye Diwani wa Viti Maalum CCM Njombe STELLA FRANCIS amesema Mgaya amewapa zawadi ambayo licha ya kuwainua kiuchumi itakuwa mkombozi hasa katika ndoa zao, kwani sasa wataweza kuhudumia familia kwa kushirikiana na wanaume zao.

Kutolewa kwa vyerehani hivyo 370 ambavyo ni sawa na viwanda vidogo 92 kwa dhana ya vyerehani vinne sawa na kiwanda kimoja kidogo kunaufanya mkoa wa Njombe kuitikia vilivyo wito wa Rais DK JOHN POMBE

MAGUFULI kuhamasisha uchumi wa viwanda.
Lengo la Mkoa kupitia wanawake ni kuwa na viwanda vidogo 35 hivyo kwa vyerehani  370 ambavyo Neema amevitoa ni kwamba lengo la kimkoa kupitia wanawake limeshafikiwa.

TENMET yawasilisha hoja 14 kwa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii

Afisa Sheria wa NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo juu ya 'Participatory Land use Management' (PLUM). Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba akizungumza mara baada ya kupokea wasilisho la hoja 14 kutoka kwa wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), hoja hizo zililenga maboresho katika sekta ya elimu. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba akizungumza mara baada ya kupokea wasilisho la hoja 14 kutoka kwa wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), hoja hizo zililenga maboresho katika sekta ya elimu. Mwanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kutoka taasisi ya ACTIONAID, Bw. Karoli Kadeghe (kushoto) akiwasilisha hoja 14 kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma 
Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba akisisitiza jambo katika kikao hicho. 
Sehemu ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo wakichangia hoja katika kikao na TENMETkilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. 
Sehemu ya wabunge na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo wakichangia hoja katika kikao na TENMETkilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. 
Kikao kati ya wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo na wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kikiendelea kujadili changamoto anuai katika sekta ya elimu. 
Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. 
 Baadhi ya wajumbe na wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakichangia hoja mbalimbali katika kikao na wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.[/caption] Na Mwandhishi Wetu, Dodoma MTANDAO wa Elimu Tanzania (TENMET) umekutana na kamati ya Bunge Huduma za Jamii na Maendeleo na kuwasilisha hoja 14 ambazo wameiomba kuikumbusha Serikali kuzifanyia kazi ili kuboresha sekta ya elimu nchini. Akiwasilisha hoja hizo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo, mwishoni mwa wiki mjini Dodoma, mmoja wa wanachama wa TENMET kutoka ACTIONAID, Bw. Karoli Kadeghe aliiomba Serikali kutenga asilimia 20 ya bajeti ya taifa kwenye sekta ya elimu kama ilivyoahidi, kwani sasa badala ya bajeti kupanda imekuwa ikishuka na ndani ya miaka mitatu imepungua toka asilimia 17 hadi asilimia 15. Alisema Serikali haina budi kuwekeza zaidi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato na matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kutoka vyanzo vya ndani ili viweze kutumika kufadhili elimu ya msingi na utoaji ruzuku shuleni uzingatieb hali halisi ya mahitaji ya sasa. Bw. Kadeghe pia aliwaeleza wanakamati hiyo kuikumbusha Serikali juu ya kuanzisha mchakato wa Bodi ya Taaluma ya uwalimu itakayoongeza tija na kulinda maslahi ya walimu katika sekta ya elimu jambo ambalo kimekuwa kilio cha walimu kwa muda sasa. Aliiomba Serikali kupitia kamati hiyo kuimarisha idara ya kudhibiti ubora (ukaguzi) na ipewe mamlaka na vitendea kazi kiuhalisia ili iweze kufanya kazi yake kiufasaha, kwani bajeti ya mwisho zilitengwa bilioni 42 ambazo hazikupelekwa hadi mwezi machi. TENMET pia iliiomba Serikali kutoa kipaumbele cha bajeti kwa sekta ya elimu kama ilivyofanywa kwa sekta ya miundombinu miaka miwili iliyopita, na uzingatiwaji wa haki za watoto na kuundwa chombo maalumu cha usimamizi, utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu. Pamoja na hayo, Serikali za mitaa kutunga na kusimamia sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi wanaowanyima watoto haki ya elimu, huku wakiomba fedha za mikopo ya elimu ya juu bajeti kuongezwa na zitenganishwe na fedha za maendeleo ya wizara ya elimu, huku vigezo vya upatikanaji mikopo kupunguzwa. Aidha ombi lingine ni kutaka kuhimarishwa kwa kamati za shule, kuhamashishwa upya kwa wazazi kuchangia maendeleo ya watoto wao kielimu, kuingiza kipengele cha elimu ya mlipa kodi katika mitaala ya elimu na pia serikali kupunguza vigezo katika upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuongeza bajeti eneo hilo. Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba aliwaahidi TENMET kuzifuatilia hoja 14 walizowasilisha wanachama wa TENMET ili ziweze kufanyiwa kazi hatua kwa hatua, ikiwa ni pamoja na kuwapongeza kwa uzalendo wanaouonesha kuipigania elimu nchini. "...Kwa hiyo ndugu zangu niwaombe na niwahakikishie kama tulivyo kubaliana wakati ule...yale mambo 14 tutaendelea kuyasemea kama kamati, ili tuweze kuendelea kuboresha maendelea ni suala endelevu, sisi kama kamati tutaendelea kuiomba Serikali iwekeze fedha nyingi zaidi kwenye sekta hii ya elimu...maana hakuna mbadala wa elimu," alisema Peter Serukamba. Kamati hiyo pia iliahidi kutembelea baadhi ya maeneo yenye changamoto kielimu kwa kukagua baadhi ya shule za msingi na sekondari kujionea changamoto na hali halisi ili kuendelea kuishawishi Serikali katika uboreshaji wa bajeti ya sekta ya elimu kiujumla. Alitumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii na hasa wazazi kutokwepa majukumu kwa watoto wao, kwani hakuna mtu anayeweza kujitokeza kazi yake ni kubeba majukumu ya mazazi/walezi kwa watoto wao. "...Lazima tusaidiane kuwakumbusha wazazi kutimiza majukumu yao, haiwezekani mzazi ukazaa alafu atokee mtu wa kutimiza majukumu yako.." alisisitiza mwenyekiti huyo. Imeandaliwa; www.thehabari.com

MHE MWANJELWA AMNADI MGOMBEA UDIWANI KATA YA IBIGI, APOKEA WANACHAMA WAPYA 21

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akimvalisha kofia ya CCM kijana aliyehama Chadema wakati wa kampeni za Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa kilimo akifurahi na wananchama wa CCM wakati wa mkutano wa kumnadi Mgombea Udiwani Kata ya Ibigi Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya Bi Suma Ikenda Fyandomo, Jana Novemba 20, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Mary Mwanjelwa (Mnec) ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo amewasihi wananchi kwa kauli moja kuchagua kiongozi makini anayetokana na CCM.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa kumchagua diwani wa CCM ni dalili nzuri ya kumpongeza na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anazozifanya kwa muktadha wa kuwaletea maendeleo watanzania wote.
Mjumbe huyo wa NEC, aliyasema hayo Leo Novemba 20, 2017 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Bujinga A na B kilichopo Kata ya Ibigi, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya ambapo alimnadi mgombea Udiwani wa Kata hiyo Bi Suma Ikenda Fyandomo.
(Mnec), Mhe Mwanjelwa aliwakumbusha wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa Hawachagui ilani mpya Bali wanachagua Diwani kwa ajili ya kutekeleza ilani ya Ushindi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 ambayo wananchi waliiamini na kuichagua Octoba 25, 2015.

CHALAMILA AMNADI BARAKA KIMATA KWA WANANCHI WA KATA YA KITWIRU

Kada wa chama cha Mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho Baraka Kimata katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa
 Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Albert Chalamila akiwa jukwaani na mgombea udiwani kupitia chama hicho 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea udiwani wa kata hiyo Baraka Kimata akiwa jukwaani kuomba kura kwa wananchi wa kata hiyo.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MAKADA mbalimbali wa chama cha mapinduzi (CCM) wamemtaka mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata kufanya kazi kwa kujituma na kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza.

Akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru mtaa wa wa Kitwiru Stand kada wa chama hicho Albert Chalamila alimtaka mgombea huyo kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha atatua kero za wananchi wa kata ya Kitwiru kwa ndio waliompa dhamana ya kuwa kiongozi katika eneo hilo.

“Leo hii tunapanda kwenye majukwaa mbalimbali kukunadi kwa kutumia akili zetu na nguvu zetu sasa ukishinda sio uanze kuwaletea kiburi wananchi wa kata hii,hapo hatuta kuwa sawa kabisa hivyo nakuomba uwaheshi na kuwatumikia vilivyo wananchi wa kata ya Kitwiru ukipewa ridhaa ya kuwaongoza” alisema Chalamila