Watoto
wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho
Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.
Mkusanyiko
wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa
yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).
Wachezaji
hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa
yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.
IMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MASHINDANO TFF, BONIFACE WAMBURA
EmoticonEmoticon