PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

October 02, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MFUKO wa pensheni wa PPF umesema utawafikisha mahakamani waajiri ambao hawapeleki michango kwa wakati kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa wateja wao.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Kanda ya Kinondoni, Tanga na Pwani, Zahara Kayugwa wakati wa semina ya waajiri wa sekta mbalimbali jijini hapa.
Alisema hatua hiyo inaweza kusaidia waajiri kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
“Kwa kweli inatubidi tuchukue hatua, kwa sababu unakuta mfanyakazi anakuja kudai mafao halafu mwajiri amechangia asilimia tano tu, sasa wateja wanatuona kama sisi ni wababaishaji… hatutawavumilia tena," alisema Kayugwa.
Aidha, akifungua semina hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salim Chima, alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini, hasa katika suala zima la kukuza na kuimarisha uchumi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »