Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu)
akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa
Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi
Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki
mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili
kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali
Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo
Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa
kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba
fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa
wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro
ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania,
Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki
kikamilifu Mafunzo hayo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah.
Wakufunzi
wa Mafunzo hayo wakisikiliza hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya
Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC. Jumla ya
Wahitimu 27 toka Nchi za SADC wameshiriki Mafunzo hayo kikamilifu katika
Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa kwanza kulia) ni Mratibu
wa Mafunzo hayo, Kanali Sambulo Ndlovu toka Zimbabwe(wa pili kulia) ni
Mkufunzi toka Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart(wa
tatu kushoto) ni Mkufunzi toka Tanzania, Ahmad Mwidadi(wa pili kulia)
ni Mkufunzi toka Zambia, Mrakibu wa Polisi Nchini Zambia, Edward Njovu.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya
mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV
Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa
Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha
Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa
sita kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali
Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu
Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa
Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu
wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher
Chellah(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini
Tanzania, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kufunga rasmi
Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za
SADC(katikati) ni Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo hayo toka Nchini
Tanzania, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Pendo Kazumba.
EmoticonEmoticon