SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUWAKUMBUKA WAZEE UJENZI WA MAKAZI BORA

September 14, 2023

 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia baiskeli za watoto wenye Ulemavu zinazotumika katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Na WMJJWM,  Tarime-MARA

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeihimiza jamii kote nchini kukumbuka ujenzi wa makazi ya wazee wasiojiweza wakati huu wa mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati akishiriki katika shughuli za maendeleo

Wilayani Tarime mkoani Mara.

Akiwa kwenye  ujenzi wa nyumba ya daktari wa zahanati ya Kijiji cha Soroneta amesema Jamii inatakiwa kushiriki katika shughuli za maendeleo ili wawe na umiliki wa miradi hiyo hususan  suala la utunzaji ili idumu.

Mwanaidi amesema, Kampeni ya Amsha Ari ni moja ya juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum juu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ya Mwaka 1996 inayohimiza Wananchi kujitolea wakati wa shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

“Mimi nimekuja hapa kuamsha ari ya wananchi kuweza kujenga makazi bora na pia kusaidia watu wengi kuwa na makazi bora hasa wazee wasio na uwezo” amesisitiza Naibu Waziri Mwanaidi.

Naye Diwani wa Kata ya Nyarelo   Japheth Marwa, amesema wananchi wa kata hiyo wamekuwa na moyo na ari ya kujitolea katika shughuli za maendeleo na wataendelea kujitoa ili kufanikisha miradi mbalimbali ya huduma za jamii iweze kuwasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya  Kijiji cha  Soroneta Kata ya Nyarelo Dkt. Richard Kitende ameishukuru Serikali  kwa kuunga mkono juhudi za wananchi kutekeleza miradi ya Maendeleo kwani inasaidia kuwapa moyo wa kujitoa na kusaidia upatikanaji wa huduma muhimu karibu na maeneo yao.

Akizungumzia hatua hiyo, Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara amesema ni jambo jema viongozi kuonesha mfano kwenye masuala ya maendeleo na jamii kwani itasaidia kuwa na moyo na mwamko kwa wananchi kuchangua katika shughuli za maendeleo.

Awali, Afisa Maendeleo ya Jamii Janeth Michael alisema mradi huo umeshirikisha wananchi kwa shughuli za kuchimba msingi, kusomba mawe na kujenga boma ambapo gharama zote za nguvu ya wananchi ni shillingi Millioni 8.1 huku wakiungwa mkono na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime iliyotoa shillingi Millioni 20 kuunga mkono juhudi za Wananchi.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia baiskeli za watoto wenye Ulemavu zinazotumika katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akisoma mabango ya ujumbe mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Kituo cha ATFGM Masanga kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati wa ziara yake mkoani Mara

  

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Kijiji cha Seroneta Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akihamasisha wananchi kujitolea katika shughuli za Maendeleo na ujenzi wa Makazi Bora wakati wa ziara yake mkoani Mara

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Kijiji cha Seroneta Halmashauri ya Wilaya ya Tarime akihamasisha wananchi kujitolea katika shughuli za Maendeleo na ujenzi wa Makazi Bora wakati wa ziara yake mkoani Mara 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi meza za vyereheni vilivyotolewa na Shirika la  Care Foundation kwa Kikundi cha  wakati wa ziara yake mkoani Mara Septemba 13, 2023.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »