Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akichangia mada katika ajenda zilizolenga kuangalia namna nchi za Afrika zinaweza kuondokana na changamoto ya nishati pamoja na kuleta mageuzi ya kilimo barani Afrika, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea Kusini Mheshimiwa Togolani Mavura, na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, (kulia), wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifuatilia mada wakati wa mkutano wa Mawaziri uliokuwa ukiangazia namna ya kukabiliana na changamoto ya nishati pamoja na kuleta mageuzi ya kilimo barani Afrika, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC), mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini. Tanzania imeungana na nchi nyingine 54 za Afrika kushiriki katika mkutano huo.
Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melcksedeck Mbise (kushoto), wakifuatilia mawasilisho wakati wa mkutano wa Mawaziri uliokuwa ukiangazia namna ya kukabiliana na changamoto ya nishati pamoja na kuleta mageuzi ya kilimo barani Afrika, katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Kamishna Msaidizi Idara ya Madeni, Bw. Nuru Ndile na Mshauri wa Uchumi, Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea Bw. John Masuka (kushoto), wakifuatilia mawasilisho katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea Kusini Mheshimiwa, Togolani Mavura, akijadili jambo na Mshauri wa Uchumi, Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea Bw. John Masuka (kulia), kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri katika mkutano wa saba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Busan, Jamhuri ya Korea Kusini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – WF, Busan, Jamhuri ya Korea Kusini)
EmoticonEmoticon