PROFESA JOHN SHAO AZUNGUMZIA UZOEFU WAKE KATIKA MASUALA YA TIBA: NI KWENYE SEMINA YA WCF KWA MADAKTARI

February 22, 2018
R
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Moshi
DAKTARI bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, ameelezea uzoefu wake  juu ya mahangaiko waliyokumbana nayo wafanyaakzi walioumia wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi inapofikia muda wa kulipwa fidia.
Akitoa uzoefu huo mbele ya madaktari wanaoshiriki mafunzo ya siku tano (5) ya tathmini ya Mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 21, 2018, Profesa Shao ambaye kwa sasa amestafu kazi, alisema uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), utawezesha wafanyakazi walioumia kazini kwa mazingira mbalimbali waweze kupata haki zao stahiki.
Ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa kufanya tathmini wakati huo, kulipelekea shida nyingi kwa wafanyakazi waliopata madhara kazini.
Aidha Profesa Shao ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi za tiba akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC Moshi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, na pia aliwahi kufanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Karatu, aliushauri Mfuko katika kutekeleza majukumu yake ni lazima sasa ujikite katika mambo ambayo aliyaona wakati huo yakiwa na mapungufu.
“Kuwe na utaratibu katika ngazi ya vituo vya afya vya binafsi na vya serikali ambavyo vitawapokea wagonjwa kama hawa na kuwapima kutokana na jinsi walivyoumia na kuwapatia rufaa ya kwenda katika hospitali za wilaya, mkoa au hizi za madaktari bingwa ili waweze kupata huduma hiyo na vile vile kutathminiwa kwa usahihi.” Alisema.
Alishauri kuwa kazi hii ya kufanya tathmini isiachiwe kwa Daktari mmoja au muuguzi mmoja au afisa mmoja tu bali pawepo na kikundi (team work) ambacho kimepata mafunzo mazuri kinachoweza kupima na kutoa muelekeo mzima na katika kufanikisha hili lazima pawepo na mfumo mzuri endelevu wa mafunzo kama haya.
“Uwepo mfumo wa wataalamu (madaktari) wanaopata mafunzo haya watoke kila kada ili wapatiwe mafunzo stahiki ya kuwahudumia wagonjwa wanaopata madhara yatokanayo na kazi, ili wawe na uwezo wa kutoa tathmini iliyo sahihi.
Pia alishauri kuwepo na mfumo wa kuimarisha uanzishwaji viwanda walau kuwe na Minimum Standard ya viwanda vinavyoanzishwa vikidhi mazingira salama ya kazi na hatua hiyo iende sambamba na mafunzo kwa wafanyakazi walioajiriwa wawe na muda wa kupewa elimu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye mazingira yao ya kazi na jinsi gani wanaweza kujiepusha nayo.
Aidha gwiji huyo wa uchunguzi wa vijidudu na madawa, aliwaasa madaktari hao kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, kuongeza uwajibikaji, moyo wa kujitolea na kutojiona kama vile mgonjwa aliyeumia anatumiwa kama mojawapo ya kuongeza kipato kwa watendaji.
 Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuhudumia wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na usalama mahala pa kazi wakati wa mafunzo ya madaktari wanaojifunza namna ya kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka Kanda ya Kaskazini mjini Moshi Februari 21, 2018 
 Mshiriki akifuatilia kwa makini nasaha za Profesa Shao.
 Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Assessment Manager), wakifuatilia nasaha za Profesa Shao. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akiongoza mafunzo hayo.
Profesa Shao, (kushoto), akiteta jambo na mmoja wa washiriki.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza kufuatia mada zilizowasilishwa kwa washiriki hao.
 
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia), akisalimiana na Profesa John Shao.
 Profesa John Shao, akisalimiana na  Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), Dkt. Ali Mtulia.
 Sehemu ya washiriki.
 Profesa John Shao.
MABINGWA WANAPOKUTANA:
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina,(kulia) na Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, wakisalimiana. 
Daktari bingwa na mbobezi wa mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina, akifafanua jambo.
-- Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.o.box 77807 Dar es Salaam, Tanzania Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033 Blog: khalfansaid.blogspot.com

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »