Na Victor Masangu, Chole Kisarawe
WAKINAMAMA
wajawazito katika kijiji cha Kihare kata ya Maluwi Wilaya ya Kisarawe,
Mkoani Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya
kutokana na ukosefu wa kutokuwa na wodi maalumu ya kujifungulia kwa
kwa kipindi cha muda mrefu na kuwalazimu kutembea umbari wa kilometa
15 kufuata huduma hatimaye kilio chao kimepata mkombozi baada kukamilika
kwa jengo la wazazi.
Aisha
Ramadhani na Fatma Iddy ni baadhi ya wakinamama ambao walisema kwa
miaka mingi wamekuwa wanateseka pindi inapofika wakati wa kujifungua
kutokana na zahanati ya Kihare ambayo walikuwa wanaitumia katika kupata
huduma ya matibabu ilikuwa haina jengo la wodi ya wazazi hivyo ilikuwa
inawalazimu kufunga safari ya umbari wa kilometa 15 kwa kutumia usafiri
wa baiskeli,pikipiki au wakati mwingine kutembea kwa miguu.
Walisema
kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua
kutokana na kutokuwepo kwa wodi ya kujifungulia hivyo walikuwa
wanachanganywa na wagonjwa wengine wa kawaida kitu hali ambayo ji hatari
kwa afya zao na mtoto, hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na
juhudi za Mbunge wa jimbo lao kwa kuamua kujenga jengo hilo ambalo
litakuwa ni msaada mkubwa katika utoaji wa huduma.
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu amekiri
kuwepo kwa changamoto ya wakinamama wa kijiji cha Kihare kutembea
umbari mrefu wa kilometa 15 kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya
kujifungua katika kituo cha afya chole,ambapo kwa sasa wameanza harakati
za ujenzi wa wodi kwa kutumia za halmashauri pamoja na michango ya
wananchi.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amebaini kuwepo kwa hali
hiyo wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya
wazazi katika zahanati ya Kihare ambapo amesema kwamba katika
kukabiliana na changamoto hiyo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5
kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya.
Jafo
alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni
kuhakikisha inaborsha sekta ya afya hivyo ujenzi wa vituo hivyo vya afya
vitaweza kupunguza adha ya wagonjwa hususan kwa wakinamama
wajawazito kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.
“Kwa
kweli katika hili la wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata shida
kubwa sana, kwani wakti mwingine wanasumbuka ya kufuata huduma ya afya
kwa kutembea umbali mrefu, hivyo tumetenga fedha kiasi cha shilingi
milioni 500, kwa kila ujenzi wa kituo cha afya kimoja nah ii kwa kweli
itapunguza sana adha ya wakinamama waliyokuwa wakiipata pamoja na
wananchi wote kwa ujumla,”alisema Jafo.
Waziri
Jafo akiwa katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Kisarawe Mkoani
Pwani ambapo ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo
sekta ya elimu, miundombinu, afya maji, pamoja na kuweza kukutana na
viongozi, watendaji , pamoja na kungumza na wananchi wa
vijiji,vitongoiji, kata kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto
wanazokabiliana nazo kwa lengo la kuweza kuzitatua.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akizungumza na baadi ya
viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa
ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya
maendeleo katika sekta ya afya, maji, barabara, pamoja na elimu pamoja
na kuzungumza na wananchi.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi na madaktari wa halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi
mbali mbai ya maendeleo pamoja na kuzungumz na wananchi.(PICHA ZOTE NA
VICTOR MASANGU)