Kiongozi
waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwa katika darasa la Shule ya
Msingi Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini
alipotembelea shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani
wa Chama hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kutoa bati za madarasa
mawili.
Kiongozi
waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia), akiwa na diwani wa
chama hicho, Hamisi Msangule (kulia) pamoja na viongozi wa ngazi
mbalimbali wa chama hicho wakitoka kwenye darasa la Shule ya Msingi
Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini alipotembelea
shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani wa Chama
hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kuchangia bati za madarasa mawili.
Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati), akiwa na viongozi
wa chama hicho wa Mkoa wa Morogoro na Jimbo la Morooro Kusini Mashariki
kwenye eneo la mto Lugwazi ambako mradi wa barabara utapita kwa kumwagwa
zege kwenye eneo hilo, ambako Chama hicho kimechangia mifuko 20 ya
saruji kati ya 60 inayohitajika.
Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa kwenye usafiri wa bodaboda
wakati akienda kukagua miradi ya maendeleo ya Kata ya Tomondo Jimbo la
Morogoro Kusini Mashariki jana.
Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Viongozi wa chama hicho mkoa
wa Morogoro Wilaya na Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wakimsaidia
mkazi wa Kijiji cha Vuleni kuandaa mahindi wakati wakiwa kwenye ziara ya
kukagua miradi yamaendeleo kwenye kata ya Tomondo inayoongozwa na chama
hicho.
Viongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe kuangalia chanzo
cha maji kinachotumika na wakazi wa Kijiji cha Vuleni Kata ya Tomondo
ambako chama hicho kimeahidi kuchimba visima virefu kila Kijiji haraka
iwezekanavyo.
…………………
WAKAZI
wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro Kusini Mashariki
wiki hii imekuwa ni ya neema kwao kutokana na kupata ufumbuzi wa baadhi
ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo.
Kata
hiyo inayoongozwa na diwani wa chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule
jana ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na
Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto za maendeleo.
Changamotokubwa
ambayo imepewa kipaombele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji
inayowakabili wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho imeahidi kuwapeleka
wataalamu wa kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi
huu.
Akizungumza
kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo jana Kiongozi wa chama
hicho, Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza
kero hiyo haitakuwa na aana tena chama hicho kupewa dhamana tena
kuongoza.
“Chama
chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo
kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao, alisema.
Mbali
ya ahadi ya kumaliza kero ya maji kiongozi huyo pia amechangia mifuko
ishirini ya saruji kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara
inayokatiza kwenye mto Lugwa kwenye Kijji cha Vuleni.
Neema
iliendelea kuwaangukia Kijiji cha vuleni baada ya Kiongozi huyo kuahidi
kuchangia bati zote zitakazo hitajika kukamilisha ujenzi wa madarasa
mawili kati ya saba yanayohitajika shuleni hapo, yatakapoanza kujengwa.
Awali
akitoa maelezo kwa Kiongozi huyo, diwani wakata hiyo, Hamisi Msangue
alisema, Kata hiyo kwakuwa ni mpya ina changamoto nyingi hivyo
kunahitajika nguvu nyingi ili kuweza kufanikisha maendelo na kutekeleza
ahadi walizoahidi wananchi.
Diwani
huyo aliwaeleza viongozi wa chama hicho kuwa zahanati yao ina manesi
wawili tu na haina mganga jambo linalowaletea usumbufu wa kupata huduma
za afya kwa wananchi.
Aidha
changamoto nyingine nyingi zilielezwa kuwa zinahitaji ufuatiliaji kwa
mamlaka zinazohusika kwaajili ya kupata majibu na kuahidi kupeleka
mrejesho haraka iwezekanavyo.
Kata
hiyo kama zilivyo kata nyingi za mkoa wa Morogoro nayo haikuachwa nyuma
kwenye migogoro ya aridhi, kutokana na wanachi wengi kumlalamikia
mwekezaji wa kizungu anaemiliki hekta 600 za Kijiji hicho bila ya kufata
taratibu.
Ziara za Chama hicho kukagua maendeleo kwenye kata zinazoongozwa na madiwai wa chama hicho zinaendelea.