Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga
akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na
katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi
waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia
misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakifuatilia mijadala anuai katika mkutano huo. |
MTANDAO wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi
leo umekutana na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana
masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa
kijinsia katika siasa na uongozi nchini.
Akiwasilisha
mada kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano huo, mtoa
mada na mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga aliwataka wanahabari
kuangalia mfumo mzima wa siasa za vyama vingi na nini kinachoitenganisha
siasa ya Tanzania na nchi nyingine bila kujali tofauti za itikadi za
vyama kwenye masuala yanayohusu utu wa mwanamke, ushiriki wa mwanamke
kuchangia fikra za siasa na uongozi.
Aliwataka
kuchambua na kuangalia mambo yapi yatakayounganisha wanasiasa wote
katika kutetea masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utu na haki za
mwanamke na pia mfumo wa uongozi utakaowezesha vyama vya siasa
kuimarisha demokrasia shirikishi yenye mrengo wa jinsia ndani ya vyama.
Pia
kuchambua mfumo wa uongozi unaowezesha vyama kutatua migogoro ndani ya
vyama vyao bila kutumia vitisho, na hususani vinavyoashiria kumsababisha
mwanamke wa Tanzania asipende kushiriki katika shughuili za siasa au
anaposhiriki ajisikie yuko salama.
Kwa upande
wake Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia
Mukurasi akizungumza katika majadiliano hayo, alisema malengo ni
kujadili kwa pamoja umuhimu wa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia
katika masuala ya siasa na uongozi nchini nchini.
Kujenga
makubaliano ya pamoja jinsi waandishi wa habari watakavyochechemua
umuhimu wa kuzingatia misingi ya jinsia kwenye masuala ya siasa na
uongozi katika majukumu yao, na kujengeana uwezo wa masuala ya usawa wa
jinsia na uongozi kwa ujumla.
--
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mobile:- 0717
030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com