Na Hamza Temba - WMU-Bagamoyo, Pwani
....................................................................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha
hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili
iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.
Ametoa
agizo hilo leo mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani
yake pia kuna mapito ya wanyamapori.
Dk.
Kigwangalla amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa
jumuiya hiyo ikiwemo tuhuma walinzi wake kutoka katika vijiji vinavyounda jumuiya kujihusisha
na vitendo vya ujangili. Hata hivyo alipokea ombi la Mwenyekiti wa Jumuiya
hiyo, Omari Tofiki ambaye aliiomba Serikali ichukue jukumu la kulinda hifadhi
hiyo kwa asilimia 100.
"Sisi
kama jamii tumeshindwa, tunaomba msaada wa Serikali, itusaidie kuondoa hawa
wavamizi na ikiwezekana ichukue jukumu la kulinda hifadhi hii kwa asilimia
100," alisema Tofiki.
Alisema
jumuiya hiyo ambayo ni muunganiko wa vijiji 24 inakabiliwa na changomoto kubwa
ya ujangili uliokithiri ambao umepelekea kuuwawa kwa wanyamapori zaidi ya
asilimia 90 ya waliokuwepo tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 1997.
Alisema
changamoto nyingine ni kukosekana kwa muwekezaji na mapato ya kujiendesha,
uvamizi wa mifugo ndani ya hifadhi hiyo na majungu yanayosababishwa na baadhi
ya wananchi na viongozi wanaonufaika na vitendo vya ujangili na uharibifu wa
hifadhi hiyo.
Dk.
Kigwangalla alisema jumuiya hiyo imefeli katika kila eneo jambo ambalo
linalazimu kuanzishwa kwa mchakato wa kuirudisha Serikalini ili iweze kuhifadhiwa
vizuri. Alitoa wito kwa viongozi wa Wilaya na vijiji kuanza kuwaelimisha
wananchi juu ya umuhimu wa kupandishwa hadhi jumuiya hiyo kwa faida ya pande
zote.
"Nimepokea
maombi mengi ya kuongeza idadi ya wanyamapori katika hifadhi ya Saadan, tatizo
kubwa hapa ni kwamba wanyamapori wanapotoka nje ya hifadhi hiyo na kupita
kwenye eneo la Wamimbiki wanavunwa na majangili ambao wengi wao wanasuply
(wanasambaza) nyamapori Jijini Dar es Salaam," alisema Dk. Kigwangalla
akielezea umuhimu wa kupandishwa hadhi hifadhi hiyo.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania TAWA, Abraham Julu amesema Serikali imekuwa ikisaidia
katika ulinzi wa eneo la jumuiya hiyo kwa kushiriki kwenye doria mbalimbali
ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kuondoa makazi ndani ya hifadhi hiyo.
Alisema
eneo hilo ni muhimu sana kwa uhifadhi wa wanyamapori kwa kuwa ni moja ya eneo
la mazalia ya wanyamapori na shoroba nne (mapito ya wanyamapori)
zinazounganisha hifadhi ya Taifa ya Saadan, Mikumi na Pori la Akiba la Selous.
Katika
hatua nyingine baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan, Dk. Kigwangalla
ameuagiza uongozi wa TANAPA kupitia hifadhi hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa
Wilaya ya Bagamoyo na vijiji kuweka utaratibu maalum utakaowawezesha wananchi
kupita katika barabara zilizopo ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya shughuli za
kijamii ikiwemo kuwatengenezea vitambulisho maalum.
Ametoa
agizo hilo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwan Kikwete kuwa wananchi wake wanazuiliwa kutumia barabara hizo
kwa madai ya kushiriki kwenye vitendo vya uharibifu wa hifadhi hiyo.
Amewataka pia viongozi wa hifadhi hiyo ya pekee barani Afrika ambayo ipo katika fukwe za bahari ya Hindi kuwa wabunifu zaidi kwa kuanzisha bidhaa mpya za utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo. Alisema hifadhi hiyo ambayo ipo karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanga ni fursa nzuri kwa watalii kutumia ukaribu huo kuweza kuwaona wanyamapori mbalimbali wakiwemo Simba, Twiga na Tembo pamoja na utalii wa fukwe.
Amewataka pia viongozi wa hifadhi hiyo ya pekee barani Afrika ambayo ipo katika fukwe za bahari ya Hindi kuwa wabunifu zaidi kwa kuanzisha bidhaa mpya za utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa zilizopo. Alisema hifadhi hiyo ambayo ipo karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanga ni fursa nzuri kwa watalii kutumia ukaribu huo kuweza kuwaona wanyamapori mbalimbali wakiwemo Simba, Twiga na Tembo pamoja na utalii wa fukwe.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori Wamimbiki wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua
migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa
Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika
wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa
TANAPA, Martin Loibooki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya Hifadhi
ya Taifa ya Saadan na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Stephano Msumi wakati wa
ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani Jana. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Saadan katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Jana.
Katikati ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA, Martin Loibooki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mazingira ya fukwe ya
Hifadhi ya Taifa ya Saadan na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete
wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya hifadhi katika wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani Jana.
Picha ya pamoja