WAZAZI WASIOFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO CHANZO CHA KUFELI KWA WATOTO WAO

January 16, 2018
 Mratibu wa Asasi ya Kiraia ya Jijini Tanga “Tree of hope” Goodluck Malilo wakati wa akitoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Komsala Kata ya Mgambo wilayani Handeni kuhusiana na mradi wa uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu ambao umefadhiliwa na Shirika la The Foundation For Civili Society ambao unatekelezwa kwenye vijiji vine vya Michungwani, Kwedizinga, Kabuku Nje na Komsanga wilayani Handeni
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo
 Kikundi cha Burudani cha Kabuku Sanaa Group wakitumbuiza kwenye mkutano huo wa uhamasishaji
Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo

WAZAZI na Walezi ambao wamekuwa wakishindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni wamedaiwa kuwa chanzo cha kupelekea matokeo mabaya ikiwemo wengine kupata sifuri katika mitihani yao.

Hayo yalisemwa leo na Mratibu wa Asasi ya Kiraia ya Jijini Tanga “Tree of hope” Goodluck Mwalilo wakati wa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Komsala Kata ya Mgambo wilayani Handeni kuhusiana na mradi wa uwajibikaji wa jamii na mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu.

Mradi huo umefadhiliwa na Shirika la The Foundation For Civili Society ambao unatekelezwa kwenye vijiji vine vya Michungwani, Kwedizinga, Kabuku Nje na Komsanga wilayani Handeni

Alisema vitendo vya wazazi kushindwa kuwajibika kwa kufuatilia
maendeleo ya watoto wao shuleni licha ya kusababisha matokeo mabaya lakini pia limekuwa likisababisha kuwepo kwa utoro wa mara kwa mara ambao umekuwa tatizo kubwa la kupelekea kushindwa kupata elimu bora ambayo ingeweza kuwasaidia kwenye maisha yao.

“Ndugu zangu wananchi mnawajibu mkubwa wa kuhakikisha mnafuatilia maendeleo ya watoto wenu shuleni kwani hii ndio inaweza kuwa chachu ya wao kufikia maendeleo yao kwani mtajua changamoto zinazowakabili na kuona namna ya kuweza kuzipatia ufumbuzi haraka “Alisema

Alisema iwapo watakuwa mstari wa mbele kufuatilia maendeleo ya watoto wao itawasaidia kuweza kufanya vizuri katika masomo yao jambo ambalo linaweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwao.

“Lakini mafanikio mazuri ya wanafunzi shuleni yanatokana na
ufuatiliaji wa wazazi,walezi na walimu ambao wakisaidiana kwa pamoja itakuwa chachu kubwa ya kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa vijana wao “Alisema.

Hata hivyo alisema licha ya hivyo lakini pia wananchi wanapaswa kufuatilia na kuhoji ruzuku zinazopelekwa kwenye shuleni zao ili kuona namna ambavyo zimetumika kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa kwa lengo la kuwa chachu ya kupata maendeleo kwenye sekta ya elimu.

Alisema licha ya kufuatilia lakini pia wanapaswa kusimamia miradi inayoendeshwa kwenye shule husika ikiwemo kuifuatilia ili kuona kama inatekelezwa kwa ubora kutokana na fedha ambazo zimetolewa.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Kassim Kajembe alisema alisema kupitia elimu ambayo wameipata imewapa mwanga mzuri wa kuweza kujua namna ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na kuhoji miradi ya maendeleo itakayotekelezwa kwenye shule zao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »