Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa fikira ya kutaka
kuwa na ofisi bora za walimu katika mkoa wa Dar es Salaam imeanza
kutimia kwa baadhi ofisi kufikia hatua ya upauaji.
Akizungumza
leo katika uzinduzi ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi,
Makonda amesema sasa anapata usingizi kuona ndoto yake inanitimia ya
kuwapa ofisi nzuri za wanafunzi.
Makonda
amesema kuwa wakati alipikuja na wazo hilo alijua hali ni kazi ngumu
lakini kutokana na msukumo wa sasa chini ya Serikali ya Dk. John Pombe
Magufuli ya elimu bure inatimia.Amesema
maendeleo yeyote kwa watoto wa kitanzania yanaanza kwa walimu ambao
ndio wataweza kuzalishwa watoto hao kupata elimu na kuinuka kiuchumi.
“Mtu
mwenye umasikini hana nyumba ambayo haina bati kamwe hawezi mtu kuwa na
nyumba ya bati ili aweze kuwa na nyumba hiyo lazima apate elimu”amesema.Katika
uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa huyo amesema wanaonunua maeneo ya shule ni
kukamatwa pamoja na wanaonunua wakamatwe ambapo mtu mmoja Ajay Shohan
amekamatwa kwa kununua eneo la shule ya msingi Mapinduzi.
Katika
hafla ya uzinduzi wa upauji wa shule msingi Mapinduzi kampuni ya simu
za mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni
Hamsini (50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni
moja ya utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za
serikali na ofisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia
ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za
elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar
es Salaam.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mchango huo kwa mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam , Paul Makonda, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Halotel, Le
Van Dai amesema mchango huo ni sehemu tu ya jitihada kubwa zinazofanywa
na kampuni hiyo katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu nchini ikiwa
pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika
kuboresha maendeleo ya nchi hasa kupitia sekta ya elimu ambayo ni
muhimili wa maendeleo ya kila nchi duniani.
“Tunatambua
kuwa, huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na waalimu ni moja ya msingi
imara katika kukuza sekta ya elimu nchini, kwa kuzingatia hili tumeamua
kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa mchango
wetu wa kifedha ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za waalimu
ikiwa ni sambamba na kuboresha mazingira utendaji kazi kwa waalimu ya
kazi na kurahishisha ufanisi wao katika kuwafunza wanafunzi ambao ni
taifa la leo na kesho” alisema Dai.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea Hundi ya Milioni 50
kutoka kampuni ya Hallotel kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za walimu 402
Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa
kukamalika kwa ujenzi wa ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mapinduzi,
leo jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Mkoa wa Dar es
Salaam, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akitoa
taarifa ya hatua za mbalimbali za ujenzi wa ofisi za walimu leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa upauaji wa ofisi ya
walimu shule ya msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Benjemini Sitta akizungumza juu hatua ujenzi
wa ofisi katika manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipaua jengo la ofisi ya walimu
katika shule msingi Mapinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Kitoa Cha Polisi Magomeni, Morcase akipata maelezo kwa Ajay Shohan
aliyenunua eneo la shule ambapo Mkuu wa Mkoa aliamuru akamatwe,leo
jijini Dar es Salaam.