Baada ya kufanyika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup kwa mafanikio
katika mikoa ya Mwanza na Mbeya sasa yaongeza wigo kwa mabingwa wa mikoa.
leo jijini Mbeya kamati ya mashindano hayo imetangaza rasmi uwepo
wa mashindano ya Ndondo Super Cup itakayofanyika jijini Dar es salaam
mwezi februari kwa kushirikisha mabingwa wa mikoa ilipofanyika Sports
Xtra Ndondo Cup.
Mwenyekiti wa kamata ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amewaambia waandishi
wa habari kuwa uwepo wa mashindano hayo ni hitimisho la msimu wa Ndondo
Cup 2017 kabla ya kuzinduliwa msimu mpya mwezi wa tatu.
"Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakua na michezo
minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, na 21 mwezi februari jiji Dar
es salaam" amesema Dauda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Super Cup Gipson George
amesema hili ni jambo lingine kubwa kutoka Clouds Media kama support
ya wanamichezo wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla hususani ujio
wa viongozi wa FIFA nchini.
"Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima
kubwa tuliyopewa Duniani lazima na sisi tuwaoneshe kuthamini ujio wao"
"Shaffih Dauda amewasiliana na TFF kuona namna ya kushirikiana
kutusaidia kuwezesha kumpata rais wa FIFA kuja kwenye fainali ya Ndondo
Super Cup ndio maana tumepanga iwe tarehe 21" amesema Gipson.
Gipson ameongeza kuwa mashindano hayo yanaendana na agenda ya Rais
wa sasa wa FIFA ya kurudi chini kabisa (grassroot) mpira unapochezwa
na watu wa kawaida wenye vipaji vya hali ya juu.
Msafara wa FIFA ukiongozwa na Rais Infantino unatarajiwa kuwasili
nchini tarehe 21 na siku inayofuata watakua katika mkutano utakaofanyika
hapa nchini.
Kutangazwa kwa michuano hiyo mikubwa kwa timu za mtaani jijini Mbeya
ni heshima kwa chama cha soka cha mkoa huo MREFA ambapo mwenyekiti wake
Elias Mwanjala amesema hiyo ni bahati ya kipekee waliyopata kwenda kukutana
na Rais wa FIFA.
"Ndondo imefanyika miaka minne lakini sisi tumepata nafasi ya
kukutana na rais wa FIFA ni bahati iliyoje, lakini kikubwa ni wana mbeya
kuungana kufanikisha jambo hili kwani sio la chama cha soka bali ni
jambo la mkoa na nyie Clouds mtusaidie kupata wadhamini" amesema
Mwanjala.
Timu zitakazoshiriki Ndondo Super Cup ni mabingwa wa Mwanza timu ya
Mnadani Fc, Mabingwa wa Mbeya Itezi United na mabingwa wa Dar es salaam
timu ya Misosi Fc huku Goms United iliyocheza fainal msimu uliopita
na misosi imeongezwa kama heshima ya mkoa wa Dar es salaam kuwa mwasisi
wa mashindano hayo.
Mbali na kutangazwa kwa mashindano hayo Clouds Media imetoa zawadi
ya fedha kwa washindi wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup Mbeya
yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Mabingwa Itezi Fc wamepata milion tatu, washindi wa pili Terminal
fc milion mbili, na washindi wa tatu Tukuyu Star milion moja.
Gasper Samwel Mwaipasi wa Tukuyu Star ameibuka mfungaji bora kwa kufunga
goli tano, Frank Anthonwa Itezi United amechaguliwa kuwa kipa bora na
beki wa kushoto wa Itezi United Salum Idrisa Chau ametajwa kuwa mchezaji
bora