Katibu Mkuu wa Maliasili na
Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia) akiwa pamoja na Meneja wa
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Paschal Shelutete
wakipatiwa maelezo kutoka kwa Simon Mushi kuhusiana na ‘’canopy
walkaway’’ ambayo aina mpya ya utalii ya kutembea juu miti kwa
kutumia kamba wakati Wajumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi,
Maliasili na Utalii walipofanya ziara ya kutembelea jana Hifadhi ya
Taifa ya Ziwa Manyara kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali
zilizotekelezwa katika hifadhi hiyo.
Mbunge wa Korogwe mjini ambaye pia
ni Mjumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mary
Chatanda akichangia hoja namna ya kuboresha vivutio vya utalii ili
watalii wazidi kutembelea katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
mara baada ya Kamati hiyo kukamalisha ziara ya kutembelea Hifadhi
hiyo jana kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zilizotekelezwa
katika hifadhi hiyo. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Maliasili na
Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi pamoja na Mbunge wa Babati mjini
ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,Pauline Gekule.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na vyombo vya habari akiwa katika
daraja lililojengwa ndani ya ziwa manyara ambalo ni kivutio cha kipekee
kwa watalii ambacho hutumiwa na watalii kujionea maji asili ya moto
(majimoto) katika eneo hilo wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi,
Maliasili na Utalii ilipotembelea jana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa
Manyara.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza na wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea jana
katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kw ajili ya kuijonea shughuli
mbalimbali zilizotekelezwa na Hifadhi hiyo.
Mbunge wa Mtama ambaye ni Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye
akiwa kwenye ‘’canopy walkawaya’ ambayo aina mpya ya shughuli ya
utalii ya kutembea juu miti kwa kutumia kamba wakati kamati hiyo
ilipotembelea jana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Mbunge wa Busokelo ambaye ni
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii
Atupele Mwakibete akipongeza namna Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
ilivyofanikiwa katika kushirikisha sekta binafsi katika kuboresha
vivutio vya utalii katika hifadhi hiyo mara baada ya Kamati hiyo
kukamalisha ziara ya kutembea ndani ya hifadhi hiyo jana kwa ajili ya
kujionea shughuli mbalimbali zilizotekelezwa katika.
Mkurugenzi wa Mipango na Sera,
Dkt. Idd Mfunda akiwa kwenye ‘’canopy walkawaya’ ambayo aina mpya ya
shughuli ya utalii ya kutembea juu miti kwa kutumia kamba katika
Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA –MALIASILI NA UTALII