Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia
ameteuliwa kwa mara nyingine na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani
Africa CAF kuwa kamishna wa mechi ya Morocco na Namibia kwenye fainali
za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN itakayochezwa Jumamosi Januari 27,
2018.
Mbali
na Rais Karia Waamuzi watakaochezesha mchezo huo namba 22 utakaochezwa
kwenye Uwanja wa Mohamed V Casablanca ni Mahamadou Keita kutoka
Mali atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba
moja kutoka Msumbiji Arsenio Chadreque Maringula na mwamuzi msaidizi
namba mbili akitokea Burkina Faso Seydou Tiama wakati mwamuzi wa akiba
ni Ghead Grisha akitokea Misri.
Hii
ni mara ya tatu kwa Rais Karia kuteuliwa kuwa kamishna wa mechi
zinazoendelea za fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.
Aliteuliwa
kuwa kamishna wa mechi ya ufunguzi ambapo Morocco walicheza na
Mauritania Januari 13, 2018 na kisha akateuliwa tena kuwa kamishna wa
mechi ya Namibia dhidi ya Zambia ambayo ilichezwa Januari 22, 2018