Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Bw. Major Songoro
(kulia) wakati wa makabidhiano ya Kivuko cha MV. KAZI mapema hii leo
jijini Dar es Salaam, katikati ni Mtendaji Mkuu toka Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na baadhi ya
wananchi waliopanda Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa kwa
Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa
ikikijenga Kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja ya
mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa
Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa
ikikijenga Kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akifurahia jambo na mmoja
ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa Kivuko cha MV. KAZI kwa
Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa
ikikijenga kivuko hicho.
Baadhi ya wananchi wakiteremka
katika Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa Serikali
mapema hii leo Magogoni jijini Dar es Salaam toka Kampuni ya Songoro
Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
………………………………………………………..
Eliphace Marwa -Maelezo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi kutoka kwa
Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza
iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko hicho mara baada ya ujenzi
wake kukamilika.
Akizungumza na wananchi, Prof
Mbarawa alisema lengo la Serikali kuongeza Kivuko hicho ni kuboresha
huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni.
“Uwepo wa vivuko vitatu
kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi na ikitokea Kivuko
kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma zitaendelea kama kawaida
bila kuathiri utaratibu wa kawaida”.Alisema Prof Mbarawa.
Ameongeza kuwa ili kuendana na
kasi ya Mhe. Rais John Magufuli Wizara yake itaendelea kuboresha huduma
za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Lindi , Kivuko cha
Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani Mwanza.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa
Mgwatu alisema Kivuko cha MV Kazi kimejengwa kulingana na viwango
vinavyotakiwa Kimataifa na ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka ya Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kuthibitishwa kuwa ni
salama kwa ubebaji wa abiria na magari.
Ujenzi wa MV KAZI umegharimu
Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800
magari 22 sawa na jumla ya tani 170.
Kivuko hicho kimekabidhiwa leo
kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini
Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia
vitatu
EmoticonEmoticon