Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisaini mkataba wa kuipatia Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) fedha za kuiongezea mtaji kiasi cha
shilingi bilioni 209.5. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo
Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Sheria kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Eligius Mwankenja
(kushoto), na Mchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Said Nyenge (kulia)
wakiwaelekeza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu
Kazungu na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga, maeneo
maalumu ya kutiwa saini kwenye Mkataba wenye thamani ya Sh. 209.5
bilioni utakaoiwezesha Benki hiyo kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu
kwa riba nafuu kwa wakulima wadogo wadogo, Makao Makuu ya Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akibadilishana mkataba na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB,
Bw. Francis Assenga mara baana ya kusainiwa mkataba wa kuiongezea mtaji
Benki hiyo wenye thamani ya Sh. Bilioni 209.5 ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2021,
Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu wakionesha mkataba waliokwisha usaini
kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara
ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
Wajumbe waliohudhuria hafla ya
utiaji saini mkataba wa kuiongezea mtaji Benki ya Kilimo wenye lengo la
kuunganisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango wa mageuzi ya viwanda
wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia)
akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki hiyo (hawamo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia)
akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki hiyo (hawamo pichani).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia)
akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Benki hiyo (hawamo pichani).
Wajumbe wa Bodi wakifuatilia kwa
makini zoezi la utiaji saini mkataba wa Serikali kuipatia Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) shilingi bilioni 209.5. kwa ajili ya
kuiongezea mtaji. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TADB Bw. William
Mhoja, Mkurugenzi wa Fedha na TEHAMA – TADB Bw. Severin Ndaskoi,
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru, Mkuu wa
Idara ya Utimilifu-TADB, Bw. Adam Kamanda, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bi,
Joyce Maduhu, na Mkurugenzi wa Mikopo wa TSDB, Bw. Augustino Matutu.
…………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM- Dar es Salaam
SERIKALI imeipatia Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), shilingi 209.5 bilioni kwa ajili ya
kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo hapa nchini, leo, Jijini Dar es
salaam.
Akiongea kwa niaba ya Serikali
wakati wa tukio la utiaji saini mkataba wa makabidhiano ya fedha hizo,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu,
alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni mkopo wenye masharti nafuu
kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ni sehemu ya shilingi 800
bilioni ambazo Serikali inatarajia kuipatia Benki hiyo ili iweze kukuza
mtaji wake.
“Ninaishukuru Benki ya Maendeleo
ya Afrika AfDB kwa kuipatia Serikali mkopo wa Dola za Marekani 93.5
milioni ambazo ni sawa na kiasi hicho cha fedha cha Sh. 209.5 bilioni
kwa ajili ya kuiongezea mtaji TADB ili iweze kuwafikia wakulima wengi
zaidi kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu” alisema Dkt. Kazungu.
Alisema kuwa fedha hizo
zitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya
ujenzi wa miundombinu ya sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza
uzalishaji na tija katika kilimo ili sekta hiyo iweze kuchangia zaidi
katika ukuaji wa pato la Taifa kuliko ilivyo sasa.
“Mwaka jana kilimo ambacho
kinategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kilichangia wastani wa
asilimia 29.1 ya Pato la Taifa lakini tunataka kupitia Benki hiyo Sekta
ya kilimo iiwezeshe nchi kukua kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 7 hadi 10
katika kipindi kifupi kijacho” aliongeza Dkt. Kazungu.
Akiongea baada ya kutia saini
makubaliano ya kupokea fedha hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Bw. Francis Assenga, ameishukuru
Serikali kwa kuiongezea Benki yake mtaji utakaotumika kuendeleza Sekta
ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ufugaji nyuki.
Alisema kuwa kiasi hicho cha
fedha kitaiwezesha Benki hiyo ambayo imekwisha wafikia wakulima zaidi ya
3,700 hapa nchini, kuanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa wakulima
wadogo na wa kati ili kuinua Sekta hiyo kwa kuongeza mnyororo wa thamani
wa mazao yatokanayo na kilimo na mifugo.
Ameihakikishia Serikali kwamba
Benki yake itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa matunda ya fedha
hizo yanaonekana na kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Ras Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwakwamua wananchi wake
katika lindi la umasikini.
“Riba za Mikopo ya Benki yetu
ziko chini ikilinganishwa na Benki nyingine ambapo sisi tunatoza
asilimia 8 hadi 12 kwa wakulima wadogo na asilimia 15 kwa wakulima wa
kati wenye viwanda wakati viwango vya riba katika soko ni asilimia 18 na
wakati mwingine vinafika hadi asilimia 40.” alisema Bw. Assenga wakati
akijibu maswali ya wanahabari.
EmoticonEmoticon