Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia
Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa
alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.
Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark
kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya
kikazi chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.
Sophia Mjema akianza ziara kuzuru maeneo mbalimbali yaliyopo katika mazingira
ya chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na
timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.
Na Dickson Mulashani
Mkuu wa
wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema amekipongeza Chuo cha St Mark (Chuo Kikuu Kishiriki Cha
St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa
ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.
Akiwasili
chuoni hapo Mh. Sophia Mjema alikuwa ameambatana na ujumbe wa timu ya wataalamu
katika ngazi mbalimbali a wilaya ya Ilala akiwemo Mratibu Mwadamizi wa Polisi, Mshauri
wa Majeshi ya akiba, Mratibu wa Magereza, Mhandisi , Afisa uhamiaji, Afisa
Elimu Taaluma, Afisa mipango miji, Afisa ustawi wa jamii, Afisa wa Benki ya
NMB, Afisa Tarafa, Diwani pamoja na Mwenyekiti wa mtaa.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Mark
Dr.Peter Kopweh akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya alipokuwa akizuru
maeneo mbalimbali katika chuo hicho.
Akimkaribisha
mgeni huyo, kaimu Mkuu wa Chuo Dr.Peter Kopweh alianza kwa kuelezea historia
fupi ya chuo hicho kilichopo eneo la Buguruni Malapa jirani na shule ya msingi
viziwi, kuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha St. John’s chenye makao yake makuu
mjini Dodoma ambacho kinatoa kozi katika ngazi astashada na shahada za sanaa
katika elimu, utawala wa biashara, rasilimali watu, elimu na biashara pamoja na
theolojia mathalani shahada ya uzamili katika elimu hili kwa ushirikiano na
kampasi mama ya Dodoma.
Sambamba na
ukaribisho huo Dr. Kopweh hakusita kuelezea Changamoto zinazokikabili chuo
hicho zikiwemo za miundombinu ya barabara, usalama wa mali pamoja na wadau wake
kadhalika suala la mipaka ambayo inaonekana kuingiliwa na wakazi wanaozunguka
chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.
Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji Ilala Bw.
Benjamin Chagula wakati akiangalia namna ya kutatua Changamoto ya mipaka ya
chuo hicho inaingiliwa na wananchi wanaoishi eneo jirani.
Nae katika
hotuba yake Mh.Mjema ambaye alipata fursa ya kuzungukia maeneo kadhaa chuoni
hapo alieleza lengo kuu la kufika chuoni hapo kadhalika kupongeza uongozi wa
chuo hicho kwa jitihada zinazofanyika.
“Nimeamua
kutoka na kuja kuwaona kwani nauthamini sana uwepo wenu katika wilaya yangu
(Ilala) kwani hii ni fursa muhimu ya serikali kuwatumia wasomi hata waliopo
vyuoni kutatua Changamoto katika maeneo waliyopo, mimi nakazia hapa wilayani na
naamini ujio huu utakuwa wenye tija sana kwetu sisi pamoja nanyi kama taasisi
katika kushirikiana” alisema Mh. Sophia Mjema.
Kadhalika
akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho, Mh.Mjema
alitangza kufungua milango ya fursa kwa wasomi hao kufika ofisini kwake na
kuleta mawazo pamoja na nguvu zao ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele huku
akikazia suala la uzalendo pamoja na wito wa Mh Rais Magufuli kuhusu kufanya
kazi.
Vilevile
Mh. Mjema alikazia suala la kuimarisha misingi ya elimu ya juu kwa kuwekeza
kwenye uboreshaji wa teknolojia kwani dunia ya sasa mitandao umekuwa nyenzo
muhimu ya kupata taarifa za kitaaluma.
“Mkakati wa
kusambaza huduma ya intaneti (WIFI)
katika vyuo vikuu hapa Ilala unaendelea kwa kasi na umesimama kwa muda kutokana
na hali ya mvua lakini baada ya hali hii kila kitu kitakuwa kama
ilivyoahidiwa,lazima msome kisasa” alihitimisha.
Nae Rais wa
chuo kwa niaba ya wanafunzi wote alifikisha Changamoto zinazowakabili ikiwemo
suala la mikopo pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwani
limekuwa likidhohofisha maendeleo ya taaluma alitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya
na kuahidi ushirikiano na ofisi ya wilaya pamoja na kujitoa kutumia taaluma zao
ndani ya jamii kwa ujumla.
Akihitimisha
zoezi hili pamoja na kumshukuru Mh.Mjema kwa kufika chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa
Chuo alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Chuo hicho hasa wakati huu ambapo
milango ipo wazi kwa wanafunzi kudahiliwa vyuoni moja kwa moja huku akiwaondoa
hofu wale wanaobanwa na kazi kuwa watapata fursa ya kusoma masomo ya jioni.
EmoticonEmoticon