Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.
Kwa mujjibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.
Michezo ya Jumamosi itakuwa ni
kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa
Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati
Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6,
mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam
Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na
mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
EmoticonEmoticon