Mkurugenzi
wa Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (aliyesimama)
akisalimiana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo kabla ya kuanza kwa
mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango
mjini Morogoro.
Wajumbe
wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango
wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mjini Morogoro.
Viongozi
waliokaa meza kuu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza
la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa
mshikamano daima, mjini Morogoro.
Wajumbe
wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango
wakisikiliza kwa makini maelezo ya mafanikio ya Mkutano wa Baraza hilo
kwa mwaka 2015/2016 ambayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya
kazi, Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro.
Katibu
wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian
Kuyava, akizungumza wakati wa Mkutano wa 13 wa Baraza hilo, Mjini
Morogoro.
Mwenyekiti
wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika,
akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana
Mkapa, akitoa nen0 la shukrani baada ya hotuba iliyotolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akifungua mkutano wa
Baraza hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Wizara hiyo, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Meza
Kuu (Walioketi Mbele) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
na Mipango, Bi. Dorothy Mwanyika, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu
wa idara na vitengo wa Wizara hiyo, mjini Morogoro.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika akitoka
ukumbini alipoongoza Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara
hiyo, Mkutano unaofanyika mjini Morogoro.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).
……………..
Na Benny Mwaipaja, WFM-Morogoro
Watumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono
juhudi za Serikali za kuiletea nchi Maendeleo ya haraka kupitia falsafa
ya uchumi wa viwanda utakao iwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025 kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusimamia
matumizi yake ipasavyo.
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika
Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bi. Dorothy Mwanyika, wakati akifungua mkutano wa 13 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili.
Bi.
Mwanyika amesema kuwa Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi, yana
malengo ya kuongeza tija, ufanisi na ushirikishwaji wa wafanyakazi
katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama agizo la Rais Na. 1 la
mwaka 1970 likisomwa pamoja na miongozo mingine linavyo elekeza.
Aidha
amewataka wajumbe wa Baraza hilo kukumbuka maelekezo ya viongozi wakuu
wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, kuhusu kusimamia ukusanyaji wa mapato na nidhamu
ya matumizi ya Fedha za Umma, ili kujenga uchumi wa Viwanda na kufikia
maendeleo stahiki.
“Tuunge
mkono juhudi za Serikali kwa kutafsri maelekezo ya viongozi kwa vitendo
ili kuthibitisha msemo usemao Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo moyo wa
Serikali” alisisitiza Bi. Mwanyika.
Pia
Bi. Mwanyika amewashukuru viongozi wa Wizara hiyo kwa kufanikisha mpango
wa Serikali wa kuhamia Dodoma ambapo katika awamu ya kwanza wafanyakazi
184 wameripoti mkoani humo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa makazi. Hata hivyo amewataka watumishi hao
kushirikiana katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja.
Kwa
upande wake Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bw. Cyprian
Kuyava, amebainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na maazimio
mbalimbali ya Mkutano uliopita wa mwaka 2015/2016 kuwa ni pamoja na
kuboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kazi na
kuongezeka kwa mshikamano miongoni mwa wafanyakazi licha ya ufinyu wa
Bajeti.
Naye
Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana
Mkapa amesema Watumishi wa Wizara hiyo wako tayari kuunga mkono juhudi
za Serikali za ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na hatua ya
Serikali kuhamia Dodoma.
Mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha unafanyika kwa siku mbili
kuanzia Machi 27 hadi 28, 2017, huku ajenda kuu ikiwa kufanya mapitio ya
utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na kujadili makadirio ya
bajeti ya mwaka 2017/2018.
EmoticonEmoticon