Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya
kuangalia Mchanga uliowekwa katika Makontena kwa ajili
yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana
Stewart Hamilton
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi
na Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama Mkoani Shinyanga Waziri Mkuu
Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya
Mchanga ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali
A0227 Mtaalamu wa Madini akiweka
Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na
kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya
kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa
Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017
kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na
Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika
Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri
Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya
Kahama Mkoa wa Shinyanga
Picha zote na PMO
…………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena
mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili
kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema wanataka kuona mchanga
unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani cha dhahabu, pia
Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.” Hata hivyo
tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia
usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri Mkuu alitembelea mgodi
huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga
kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo
amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa
kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua kuchukua sampuli za
mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya
kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji
kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”
Waziri Mkuu amesema sera ya
uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya
uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo
wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili lipo
miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba
mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na
kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati huohuo Waziri Mkuu
amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na zoezi
la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha mchanga wa madini nje ya
nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika migodi na wamiliki
kutowapunguza na badala yake waache waendelee na majukumu yao.
Kwa upande wake Meneja
Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa
mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.
Alisema kwa siku wanachenjua
makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata kilo
tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.
Bw. Mkanza alisema wanazalisha
asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye
mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo
unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.
“Hapa Buzwagi tuna makontena
179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya
Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa
na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena
108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
DODOMA.
JUMANNE, MACHI 28, 2017.
EmoticonEmoticon