Mchumi
Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti
na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera
ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa
waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya
Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUMUKO
wa bei utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa
nchi, Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka
Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, ameiambia
semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo
mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.
Semina
hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu
ya Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa
habari kuhusu namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.
Chini
ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama
mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei
utokanao na ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji
katika taifa unapopungua au kuonegzeka. Sera ya fedha maana yake ni
pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na
hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.
“Inapogundulika
kuwa kiwango cha fedha ni kikubwa kwenye mzunguko kuliko uzalishaji BoT
kazi yake hapa ni kupunguza fedha kwenye mzunguko na hii sio kwa eneo
fulani tu la nchi bali ni nchi nzima ambako fedha ya Tanzania
inatumika.” Alisema Mchumi huyo.
Akifafanua
zaidi kuhusu namna BoT inavyoshughulikia ujazi wa fedha au kupunguza,
Lusajo alisema njia pkee inayotumika ni kupitia mabenki ya biashara.
“Kama
mjuavyo bei ya Mafuta inadhibitiwa na soko la Dunia, na hata mfumuko wa
bei za vyakula unategemea na tabia nchi kama ukame unaopelekea upungufu
wa chakula, hapa BoT inachofanya ni kutoa usahuri kwa Serikali ili
kupitia vyombo vyake ikiwemo vile vya kodi kufanyia kazi hali hiyo.”
Alifafanua Mchumi huyo Mwandamizi wa BoT.
Alisema
moja ya hatua za kuongeza ujazi wa fedha kwenye mzunguko ni hatua ya
hivi karibuni ya Benki Kuu, (BoT), kupunguza kiwango cha amana
zinazowekwa na mabenki ya biashara kwenye Benki Kuu, kutoka asilimia 10
hadi asilimia 8.
“Hii
ina maana asilimia 2 ambayo Benki Kuu imeondoa, sasa mabenki ya biashara
yanaweza kukopesha wananchi na hivyo ujazo wa fedha kuongezeka kwenye
mzunguko.” Alisema Lusajo.
Ieleweke
kuwa fedha ili ziongezeke kwenye uchumi lazima zipitie kwenye mabenki
ya biashara ambayo yatazitoa kwa wananchi kupitia mikopo. “Na mikopo
itolewayo na mabenki iko mingi sana na kwenye taasisi nyingi kama vile
SACCOS, VICOBA na hata wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wakubwa na
wadogo na watu binafsi pia, alisema
Mchmi
huyo pia alisema, Watanzania wengi hawana utamaduni wa kuweka fedha
benki ili kuziwezesha benki hizo nazo kuwa na uwezo wa kuwakopesha zaidi
wananchi.
Hata
hivyo kiwango cha fedha kinachotolewe na mabenki ya biashara hapa nchini
ni kidogo kuliko kile ambacho watu wanataka kukopa na hivyo ili mabenki
hayo yaweze kukopesha, lazima benki hizo nazo zikope kwa mabenki
mengine yawe ya ndani au nje ya nchi.
“Hivyo
benki za biashara kwa vile inapaswa kulipa riba huko ilikokopa, na
kulipa mishahara wafanyakazi wake, mtu atakayewkenda kukopa lazima alipe
riba ya asilimia 20 kwa mfano na ukimuuliza kwanini unamtoza riba hii
ya asilimia 20, atakwambia, mimi nimekopa ili niweze kuwakopesha
watanzania ambao wengi hawapendi kuweka fedha benki, alifafanua
Akifafanua
zaidi, Mchumi huyo alisema, hivi karibuni BoT, imepunguza riba kutoka
asilimia 16 hadi asilimia 12 kwa benki za biashara zinazokwenda kukopa
Benki Kuu ili ziweze kutoa mikopo kwa wananchi. Alifafanua Lisajo
Meneja
Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia
Mbeo, akifafanua baadhi ya hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari
kuhusu mada ya Sera ya Fedha.
Baadhi wa Waandishi wa habari wakifuatilia mada hiyo
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina akizunhuzma mwanzoni mwa warsha hiyo.
Bw.Genes Kimari, (kushoto), na Bw. Mohammed Kailwa wote kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha -BoT
Meneja
Masoko ya Ndani Kurugenzi ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania,
(BoT), Bw.Reverian Mbeo, akizunhuzma wakati akiwasilisha mada juu ya
Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa sera ya fedha
wa Benki
Kutoka
kulia, Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw.
Richard Malisa, Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Zalia
Mbeo, Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi,
BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, na Bw.Mohammed Kailwa kutoka Kurugenzi ya
Masoko ya Fedha, BoT.
EmoticonEmoticon