Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akieleza umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia
Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu
wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na kulia kwake waliokaa ni Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa
Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akiratibu shughuli ya uzinduzi
wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya
Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu uliofanyika Ofisi ya Waziri
Mkuu Bungeni Machi 28, 2017.
Mchumi Idara ya Uratibu wa
Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha
namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali
unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) Dodoma.
Mchumi Idara ya Uratibu wa
Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha
namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali
unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo Machi
28, 2017 Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………..
Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa
Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu ulianzishwa
kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji
kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).
Akizindua mfumo huo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo huo kuwa umejikita
katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo
yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.
“Mfumo huu utasaidia sana katika
kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa
maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona utekelezaji wake kwa
urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema Mhe.Waziri.
Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya
Waziri Mkuu kuongeza ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za
kila siku za Serikali kwakuwa taarifa zote zitapatikana kwa wakati na
takwimu za uhakika.
Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa
mfumo ni moja ya sehemu ya kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza
ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa kwa mfumo huo kutatua changamoto
za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika kwa ujumla na kuleta
ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.
Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo
umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha Mawaziri
wote, Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli
na Watendaji wa Serikali.
Kwa kumalizia Waziri alipongeza
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa
kuona umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa
Serikali kuutendea haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu
kwa Watumishi wa Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani
kupitia Mfumo huu, mzembe atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na
ikumbukwe tu, wazembe na wavivu hawana nafasi katika Serikali ya Awamu
ya Tano”.
EmoticonEmoticon