Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe akizungumza na waandishi wa
habari Mjini Dodoma (hawapo Pichani) kuhusu agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania la kuachiwa huru kwa msanii wa Muziki wa kizazi
kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe.
Anastazia Wambura.
Mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) akiwa katika pozi.
…………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
*Amshauri aboreshe wimbo wake zaidi, Amesema ni haki yake ya kujieleza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia
huru msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama
Ney wa Mitego kutokana na wimbo wake Wapo unaosadikiwa kukiuka madili.
Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya
Rais Magufuli, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
George Mwakyembe amesema kuwa Msanii huyo ametumia haki yake ya
kikatiba ya kujieleza na ni Haki ya kila Mtanzania kujieleza kwa namna
moja au nyingine pasipo kuvunja katiba ya Nchi.
Waziri Mwakyembe amesema
Mwanamuziki huyo ni Mmoja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na Mhe Rais
kutokana na kazi zake za muziki zinazoelimisha na kueleza changamoto
mbalimbali zinakumba taifa letu.
“Mhe. Rais anaupenda wimbo wa
msanii huyu na ameshauri auboreshe zaidi asipunguze chochote ila
aongezee tu tabia nyingine ambazo hajazitaja katika wimbo wake”
alisisitiza Dkt Mwakyembe.
Aidha Mhe. Waziri ameeleza kuwa
Mhe Rais ametoa ushauri kwa msanii huyo kuboreshe wimbo huo zaidi kwani
mengi aliyoyaongelea katika wimbo wake yanatokea katika jamii na kutolea
mfano kama akiboresha na kuelezea zaidi kuhusu wakwepa kodi,wauzaji,
wasambazaji na watumiaji madawa ya kulevya,na watanzania wasipoenda
kufanya kazi kwani makundi haya yote yapo katika jamii.
EmoticonEmoticon