Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesaini leseni za
madini kutoka kwa wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na
kutimiza taratibu zote zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Leseni
ya kwanza iliyosainiwa ni ya uchimbaji wa kati wa dhahabu katika eneo
la Masagalu, Handeni yenye namba ML 570/2016. Leseni hiyo imehamishwa
kutoka kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni Najim & Company Ltd
kwenda kwa Shale Investments Tanzania Ltd.
Aidha,
Waziri Muhongo alisaini leseni namba ML 572/2017 ya Sisti Mganga.
Leseni hiyo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo la
Itiso, Chamwino mkoani Dodoma.
Leseni
nyingine iliyosainiwa na Waziri Muhongo ni ya uchimbaji wa kati wa
madini ya ujenzi aina ya kokoto, ambayo mmiliki wake ni Said Abdallah.
Leseni hiyo namba ML 573/2017 ipo eneo la Chipite, Masasi.
Profesa
Muhongo aliwataka waombaji na wamiliki wote wa leseni za madini nchini,
kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo taratibu zote kama zilivyobainishwa
katika Sheria ya Madini ikiwemo ulipaji wa mrabaha na kodi mbalimbali,
kujenga mahusiano mema na jamii zinazowazunguka pamoja na kuzingatia
utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
Zoezi
hilo la utiaji saini lilifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara
mjini Dodoma na kushuhudiwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya
Nishati na Madini.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisaini
leseni za madini za wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na
kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa. Anayeshuhudia ni Mwanasheria wa
Wizara, Khadija Ramadhan.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia),
akikabidhi leseni iliyohamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali Najim
& Company Ltd kwenda kwa Shale Investment Tanzania Ltd.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia),
akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo
la Itiso – Chamwino kwa mmiliki wake Sisti Mganga. Kulia ni Kaimu
Kamishna wa Madini, Mhandisi Rayson Nkya.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka
kushoto), akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi
(kokoto) kwa mmiliki wake Said Abdallah iliyopo Chipite wilayani Masasi.
Wanaoshuhudia (kulia) ni wataalam kutoka wizarani.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwa katika
kikao na wawekezaji mbalimbali wa madini walioomba leseni (kushoto).
Kulia ni wataalam kutoka wizarani.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akiwa katika
kikao na wawekezaji mbalimbali wa madini walioomba leseni (kushoto).
EmoticonEmoticon