PPF YAKABIDHI WA VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA WILAYANI LONGIDO, ARUSHA

March 27, 2017
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko huo, uliofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.

Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.

Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama aliungana na Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF kwenda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya Afya 16 nchini vilivyonufaika na msaada wa vifaa hivyo.

Waziri Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake. “Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio alisema msaada wa vifaa hivyo ni moja ya majukumu ya Mfuko kusaidia jamii (CSR), hivyo PPF itatoa msaada kama huo kwa hospitali na vituo vya afya vingine 15.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula,

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Juma Mhina.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Juma Mhina, wakati walipowakuwa wakiwasili katika Kituo cha Afya, Longido, kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (katikati), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Kituo cha Afya Wilayani Longido.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akimsalimia na kumjulia hali, Bi. Naseriana alielazwa katika Kituo cha Afya cha Longindo, wakati alipoambatana na Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF kwenda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo huku Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo akionekana upande wa kulia wa Mkuu wa Mkoa. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Longindo, alietambulika kwa jina la Angel Tarimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimueleza jambo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, juu ya vifaa tiba walivyovitoa katika Kituo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba kwa Kituo cha Afya Longindo. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Juma Mhina (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »