KAMPUNI MAARUFU YA FILAMU YA UJERUMANI KUPAISHA SEKTA YA UTALII NCHINI

December 01, 2016


Moja ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara  na inatarajiwa kukuza utalii .

Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha(kushoto)Gabriel na Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouder wakiwa eneo la kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi.

Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouderk(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati) anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha,Gabriel.

Mratibu wa Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Mona Lessink akizungumza na waandishi wa habari kuhusu filamu hiyo itayoanza kurushwa katika kipindi cha Pasaka mwaka 2017,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal shulutete akifatilia kwa karibu.

Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni

Wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa eneo la kutengeneza filamu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti

Askari wanyamapori wa  Hifadhi ya Taifa Serengeti wakiimarisha ulinzi kwa wageni hao

Katika kuboresha filamu hiyo upigaji wa picha kwa kutumia ndege ndogo ili kuonyesha madhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ulifanyika chini ya usimamizi wa Tanapa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »