Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya
Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS).
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya
Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS)
(hawapo pichani).
Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya
Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS)
(hawapo pichani).
Baadhi
ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani).
Semina
ikiendelea kwa wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani).
Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam,
Jane Mwajalebela.
Baadhi
ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi
ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack.
Baadhi
ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi
ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack.
KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa laini maalumu za simu za mkononi kwa
ajili ya wanafunzi wa vyuo zitakazokuwa na gharama nafuu za matumizi ya
mtandao wa intaneti na ofa mbalimali za matumizi ya simu kuwawezesha
wanafunzi kutumia mtandao kwa masomo yao.
Akizungumzia
ofa hiyo maalum iliyotangazwa kwenye semina kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Biashara Mlimani wa mwaka wa kwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara
Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela alisema ofa hiyo kwa wanafunzi
wa chuo imetolewa baada ya TTCL kusikiliza ombi la wanafunzi juu ya
kupunguziwa gharama hasa kwenye intaneti kwa kuwa hutumia mtandao huo
kujipatia masomo.
Bi.
Mwajalebela alisema laini hizo kwa wanafunzi ambazo zinajulikana kwa
jina la 'Boompack', ambapo wanafunzi wa chuo watakuwa na fursa ya kupata
huduma za vifurushi vya bei nafuu, ujumbe mfupi wa simu 'SMS' za
kutosha na muda wa maongezi ambao kiujumla utarahisisha huduma kwa
matumizi yao.
"leo
na Hivyo basi, tunapenda kuwatangazia kuwa TTCL inatoa laini za
wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack, wanafunzi wanafursa
ya kupata huduma za vifurushi vya bei nafuu, SMS za kutosha na muda wa
maongezi. Laini hii ni maalumu kwa wanafunzi na tumeanzisha ili kutoa
fursa kwa wanafunzi kutumia intaneti kwa ajili ya kushughuli za kimasomo
na kuimarisha mawasiliano miongoni mwa wanafunzi.
Pia,
tumeongeza radha zaidi wanafunzi waweza kuchagua vifurushi vya Siku,
Wiki na Mwezi. Zaidi na zaidi, Kwa wanafunzi watakajiunga na kifurushi
chochote watapata fursa ya kuperuzi facebook, Instagram, Whatsapp na
E-mail Bure," alisema Bi. Mwajalebela. Aliongeza kuwa TTCL inaamini kuwa
wanafunzi watatumia huduma hiyo kikamilifu ili kuimarisha mawasiliano
miongonu mwao, kutumia intaneti kwa ajili ya kutafuta taarifa za
kimasomo, kupata taarifa za maendeleo na kutumia fursa hiyo kuongeza
wigo wa maarifa kwa kushirikiana na vyuo vingine ndani na nje ya
Tanzania.
Awali
ya yote, naomba kuchukua nafasi hii kushukuru sana Uongozi wa DARUSO-
University of Dar es salaam Business School (UDBS) kwa kutualika TTCL
ili tuweze kushiriki nanyi kwenye tukio la leo la kuwakaribisha
wanafunzi ambao wamejiunga Mwaka wa Kwanza.
Kwa
niaba ya Menejimenti ya TTCL, inapenda kuwapongeza kwa kujiunga na Chuo
Kikuu cha Dar es salaam, tunaamini ni fursa yenu pekee ambayo mnapaswa
kuitumia kikamilifu ili muweze kujijenga wewe binafsi na kutumia elimu
hiyo kujenga Taifa letu. Pia, tunafarijika sana kuona wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam kupitia DARUSO-UDBS kutuamini na kutambua
mchango wa TTCL katika kuimarisha mawasiliano ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania, kukuza uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
Tunaimani
kuwa wanafunzi na uongozi wa Chuo mtakuwa mstari wa mbele katika
kutumia huduma za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Alisema Kampuni ya
Simu Tanzania(TTCL) ilianzishwa mwaka 1994 ambapo inamilikiwa na
serikali kwa asilimia 100. Kampuni hii inatoa huduma za mawasiliano ya
simu ya mezani, simu za mkononi na intaneti kwa wateja wa ndani na nje
ya mipaka ya Tanzania. Kampuni hii imekuwa mhimili mkuu wa mawasiliano
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Na
hii inatokana na uwezo wake wa kuunganisha nchi za jirani kupitia
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo TTCL ndio Msimamizi kwa niaba ya
Serikali. Nchi hizo ambazo zimeunganishwa kwenye Mkongo wa Tafa ni
pamoja na Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya, Malawi na Zambia. Aidha,
Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inamiliki Kituo cha Mawasiliano cha
Intaneti- TTCL IP-Pop ambacho kinatoa huduma ya intaneti kwa wateja
kutoka ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania. Kituo hiki kimekua
msaada mkubwa, hivi sasa Intaneti inapatikana hapa hapa Tanzania hakuna
tena haja ya kwenda kununua intaneti Ulaya au kwingineko. Alisema kuwa
TTCL ni kampuni pekee yenye mtandao ambao umeenea nchi nzima, hivyo
kutoa fursa kwa taasisi za Umma na Binafsi kutumia miundombinu hiyo
kukuza biashara na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi.
TTCL
imefanikisha kuuganisha Taasisi za Umma na Binafsi katika Mkongo wa
TTCL ambao umeunganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; wateja
hao ni pamoja Taasisi za fedha-Benki, watoa huduma za Afya, watoa huduma
za elimu, watoa huduma za Mawasiliano (service providers), watoa huduma
za usafiri, wafanyabishara wadogo na wakati (SMEs).
Mwaka
2014, Kampuni ilianza kutekeleza mkakati kabambe wa kuleta mageuzi
ndani ya kampuni, kuongeza uwajibikaji, kukuza biashara na kuboresha
miundombinu ya mawasiliano. Mkakati huu umekuwa na manufaa kwa Kampuni
kutokana na kufanikiwa kuboresha huduma za simu za Mkononi. Hivi sasa
Kampuni hii inatoa huduma za simu za mezani, simu za mkononi na huduma
ya intaneti. Kwa simu za mkononi ambazo vijana wengi wanatumia zaidi,
TTCL
inatoa huduma hiyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya 4.5G ambayo
inatoa intaneti yenye kasi zaidi, bei nafuu na bora zaidi. Pia, wateja
wetu wanapata fursa ya kupiga simu kwa bei nafuu zaidi. Huduma hii
tumeanza katika jiji la Dar es salaam na tuko kwenye mchakato wa
kukamilisha huduma hiyo katika jiji la Mwanza, Arusha Mbeya na Dodoma
pamoja na mikoa mingine itafuata.
EmoticonEmoticon