Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John
Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa
jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili
kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani
Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki
usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina
Mageni Lutambi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa
kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku
wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada
ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese
Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
Askari polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao
za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP
Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya
Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo
umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la
polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa
akiishi maeneo ya VETA mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na
wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe. Baada
ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese Mkoani Katavi
kwa ajili ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la
polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba
mwili huo kutoka hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo
umefikishwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa
leo (01/12/2016).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina
Mageni Lutambi akiwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na
familia kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida
SSP Peter Charles Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja
na wafiwa na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP
Mayalla Towo akiwashukuru wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki
msiba huo, Towo amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha
na kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.
Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
Na Mathias Canal
Mwili wa Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew Mtigumwe.
Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe
30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa
wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi
1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari
Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma
katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987.
Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti
wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi
(2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008),
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015)
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi
ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa
Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa
mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa
wa Singida.
Kufuatia
kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole
kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
EmoticonEmoticon