Anayeongea kwa vitendo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Bank Kuu tawi la Zanzibar mara baada ya kutembelea taasisi hiyo ya muungano mjini Unguja.
Bi Safia Hashim, Mtengenezaji na Muuzaji wa mapambo na sabuni zitokanazo na zao la mwani, mdau anayefadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH taasisi ya muungano iliyopo chini ya wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania tawi la Zanzibar, akimuelezea Naibu Waziri Mpina faida na matumizi ya zao la mwani na kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho yaliyoandaliwa na taasisi hiyo mjini Unguja wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi watumishi wa tume ya sayansi tawi la Zanzibar. COSTECH alipotembelea taasisi hiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar. (Picha zote na Habari na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
EVELYN
MKOKOI
AFISA
HABARI
OFISI
YA MAKAMU WA RAIS
HABARI
KUTOKA ZANZIBAR
Naibu Waziri Ofisi ya
Makmu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameendelea na ziara yake Mjini
Ugunja na kutembelea taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Bank kuu
ya Tanzania tawi la Zanzibar na Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyopo
chini ya Wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya uwasilishwaji
wa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank kuu tawi la Zanzibar, na Naibu
Gavana wa Bank hiyo Dkt. Natu Mwamba, Bw. Mansour Abdalla
Meneja wa fedha na utawala wa Bank hiyo tawi la Zanzibar alieleza kuwa
dhana ya ajira kwa watumishi wa Bank hiyo kwa ni ya upendeleo na kujuana
haina ukweli wowote kutokana na sababu kuwa taratibu ajira za Bank hiyo
zimewekwa pamoja katika makao makuu ya Bank hiyo jijini Dar es Salaam
na huwa nafasi za kazi hutangazwa katika magazeti na wananchi wenye
vigezo kupata kazi.
“wananchi wajenge
tabia ya kusoma magazeti hasa kwa wale wanaotafuta ajira katika bank
hii kwani kazi za hapa huwa zinatangazwa huko na bank inatoa ajira bila
upendeleo na kwa upande wa Zanzibar asilimia 48% ya watumishi ni wazanzibari
na asilimia inayobakia ni ya upande wa pili wa Muunano.” Alisisitiza
Bw. Mansour.
Akitolea ufafanunuzi
suala la mgawo wa asilimia 4.5% ya mapato ya Bank hiyo kwa Zanzibar
kama sehemu ya Muungano, Mkurugenzi wa Fedha wa Bank hiyo Tawi la Zanzibar
bw. Jamhuri Ngelime alisema kuwa hana Jibu la moja kwa moja kuhusu mgao
huo ila serikali hizi mbili za muungano zilikubaliana kuwa asilimia
45% ya faida ya Mapato yote ya Bank hiyo nchini igawiwe kwa Zanzibar,
na hivyo sheria ndiyo inavyosema.
Kwa Upande wake Naibu
Waziri Mpina, aliitaka Bank hiyo kufanya bidii ili kuhakikisha inafikia
malengo ambayo serikali imejiwekea, na kuishauri bank hiyo kuongeza
huduma zake za ki bank hasa kwa upande wa Pemba na kuweka masharti nafuu
kwa wafanya biashara wenye ma bank, ili kuweza kutoa huduma hiyo na
kuondoa gape ya kifedha iliyopo kati ya Unguja na Pemba.
Wakati
Huo Huo,
Naibu Waziri Mpina aliitembelea
Tume ya Sayansi na Teknolojia tawi la Zanzibar COSTECH na katika majadiliano
na watumishi wa tume hiyo Naibu Wazri Mpina alisema kuwa tafiti za kisayansi
ni muhimu sana kwa nchi yoyote duniani kuendelea, nchi haiwezi kuingia
kwenye Biashara ya Gas na oil bila wana sayansi kufanya tafiti zao.
Na kupongeza mchango
wa taasisi hiyo katika jamii, ikiwa ni pamoja na kufadhili wanachuo
wanasansi mbali mbali nchini.
Ziara ya Naibu Waziri
Mpina Mjini Unguja ilihusisha kutembelea taasisi za Muungano, Kumuwakilisha
Mhe. Makamu wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan katika siku ya Kizimkazi alipozaliwa Makamu wa Rais, Pamoja na
Kutembelea Ofisi zake zilizopo Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
EmoticonEmoticon