Katika Picha ya pamoja aliyekaa kati kati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina pamoja na watumishi wa Taasisi ya ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyopo Buyu katika wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kati kati ni Dkt. Yohana Shebule muhadhiri wa ya Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, na Makamu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Profesa Mtolela wakitembea kukagua jengo jipya la taasisi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, pamoja na ujumbe wake wakisikiliza taarifa na changamoto za jengo jipya la za Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, toka kwa dkt.Yohana Shebuda hayupo pichani, wakati wa kukagua jingo hilo pamoja na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kushoto Pamoja na ujumbe wake.wakiendelea kukagua jengo la Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
HABARI KUTOKA ZANZIBAR
Naibu waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa wito
kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti
hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.
Mpina aliyassema hayo,
alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu
cha DSM iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe
wa Zanzibar, iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya Elimu
Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Kukagua
jengo jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana
na changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina
aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia
wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi
wao na kuongeza pato la taifa.
Aidha, Mpina aliongeza
kwa kusema kuwa anategemea tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe
muongozo kwa serikali na namana ambavyo nchi inavyoweza kukabiliana
na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni serikali inapata
taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na hamsikiki.” Alisisitiza
Mpina.
Kwa upande mwingine
taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni toka katika
nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na kufanya tafiti juu ya viumbe
hai waishio baharini aina ya Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu
mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo na
kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia malipo ya mafunzo hayo maalum.
Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa taasisi hiyo kuwa na jengo
zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na kuwashauri wahamie
na kuanza kulitumia jengo hilo.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar
pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Samia
Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, inahusisha
pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo.
EmoticonEmoticon