Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakati wa ziara ya kupokea
miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyeweka mkono kwenye mfuko wa suruali) akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Kahama walipofanya ziara katika mgodi wa Buzwagi wa kukabidhiwa miradi ya maendeleo.
Meneja Mkuu wa Mgodo wa Buzwagi Asa Mwaipopo akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
Kifaa maalumu cha kupoza umeme ambacho kitatumika kupeleka umeme katika
mji wa Kahama na kungunguza tatizo la kukosekana kwa umeme kikiwa
kimefungwa katika kituo cha Umeme cha mgodi wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (Mwenye kofia ya blue)
akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye kofia
ya kaki) wakati wa makabidhiano ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya
Budushi, wengine katika
picha ni mbunge wa kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba na Mwenyekiti wa
halmashauri ya mji Kahama Mhe.Abel Shija.
Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu na Mbunge wa Kahama Mhe.Jumanne
Kishimba wakizindua majengo ya shule mpya ya Budushi iliyojengwa kwa
ufadhili wa mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa kijiji cha
Budushi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo
na nyumba moja ya walimu katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa Buzwagi na
Watendaji wa Kata ya Mwendakulima
Moja ya majengo ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Budushi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mwendakulima.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.
Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi uliyoko
wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, umekabidhi kwa uongozi wa
katika Halmashauri ya mji wa Kahama majengo ya shule
mpya ya msingi Budushi yenye madarasa sita, ofisi ya walimu na nyumba
moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili.
Akikabidhi
madarasa hayo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu, Meneja Mkuu
wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema ujenzi huo
umefadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi kwa zaidi ya shilingi
milioni mia nne na themani kupitia mfuko wa Acacia Maendeleo Fund,
ambao umelenga kuwapunguzia adha wanafunzi wa eneo hilo la Budushi na
maeneo yanayozunguka eneo hilo kuondokana na adha ya kutembea mwendo
mrefu kwenda shule.
Aidha,
Meneja mkuu huyo wa Mgodi wa Buzwagi alikabidhi pia nyumba mbili za
kisasa za walimu zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa shule ya msingi
Mwime hatua ambayo amesema kuwa itasaidia katika kupunguza
tatizo la nyumba kwa walimu kwa shule hiyo. Nyumba hizo ambazo
zimejengwa kwa kutumia teknolojia ya Tofali za kufungamana zimegharimu
shilingi milioni mia mbili arobaini na nane (248,126,000/=)
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea
miradi hiyo ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo
wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika
kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza
kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea
kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
EmoticonEmoticon