Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akimkabidhi msaada wa bati 100 pamoja
na madawati 100 vyote vikiwa na thamani ya Tsh milioni 7.2 mkuu wa
kituo cha Yatima cha Faraja Mgongo kata ya Nduli Manispaa ya Iringa
Padri Franco Soloberi jana , mkuu huyo ametoa msaada huo kufuatia janga
la moto lililoteketeza majengo ya kituo hicho mwezi
uliopitaanayeshuhudia kushoto ni diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
Diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtoveakimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kutekeleza ahadi yake ya madawati na bati.
Viongozi na watoto wanaolelewa kituo cha Faraja Mgogo wakimsikiliza diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
Viongozi na watoto wanaolelewa kituo cha Faraja Mgogo wakimsikiliza diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove.
RC
Iringa Amina Masenza akimkabidhi mkuu wa kituo cha yatima cha Faraja
Mgogo Padri Franco Soloberi madawati 100 kulia ni diwani wa Nduli Bashir
Mtove
Diwani wa Nduli Bashir Mtove na mkuu wa kituo cha Faraja Padri Franco wakipiga makofi kumshukuru RC Masenza kwa msaada wake.
Jengo lililoungua.
Watoto yatima wakimpongeza RC Masenza kwa msaada wake.
Wanafunzi wakiwa wamekaa katika madawati yaliyotolewa msaada na RC Iringa .
Bati 100 zilizotolewa na RC Masenza.
RC Masenza akionyeshwa ramani mpya iliyochorwa na Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kituo hicho.
Na MatukiodaimaBlog
MKUU
wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amekabidhi msaada wa madawati 100 na
bati 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 7.2 kwa kituo
cha kulea yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Faraja
Mgongo baada ya kituo hicho kuteketea kwa moto mwezi mmoja uliopita .
Akikabidhi
msaada huo leo kituoni hapo mkuu huyo wa mkoa aliyeongozana na kamati
yake ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa alisema kuwa mara baada ya
kituo hicho kuungua moto alifika kituoni hapo na kati ya ahadi alizopata
kutoa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo hicho pamoja na madawati
kwa ajili ya wanafunzi hao ahadi ambayo ameitimiza kwa wakati.
Bi
Masenza alisema kuwa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dr John
Magufuli ni serikali ya kuwatumikia wananchi hivyo akiwa ni mwakilishi
wa Rais ngazi ya mkoa ataendelea kuwatumikia wananchi na kuona hakuna
mwanafunzi anayekaa chini na ndio sababu ya kutoa madawati hayo 100 ili
kuwawezesha wanafunzi hao kusoma vizuri.
“ mkoa
wa Iringa umejipanga vizuri kuwatumikia wananchi wake na ndio maana
baada ya moto huu kuteketeza jengo la watoto hawa yatima nimekuwa bega
kwa bega na uongozi wa kituo ili kuona jengo hilo linajengwa kwa wakati “
Hata
hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema aliagiza Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa kuchora ramani mpya ambayo tayari ili majengo hayo yajengwe kwa
ustadi kama njia ya kuepusha madhara makubwa kwa watoto pindi moto
unapotokea .
“
Tunamshukuru Mungu wakati moto unatokea katika jengo hili watoto wote
hawakuwepo ndani walikuwa nje ya kituo hicho kwa ziara ya mafunzo ila
kama wangekuwepo ndani jinsi majengo hayo yalivyojengwa yawezekana
yangetokea madhara mengine kwa watoto …..ramani hii mpya itasaidia
majengo hayo kujengwa kwa kuzingatia majanga pindi yanapojitokeza kwa
watoto kutoka kirahisi zaidi”
Diwani
wa kata ya Nduli Bw Bashir Mtove pamoja na kumpongeza mkuu wa mkoa wa
Iringa kwa kuwasaidia watoto hao waliopo kata yake bado alisema bado
msaada zaidi unahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho .
Alisema
watoto hao bado wanakabiliwa na mahitaji mbali mbali yakiwemo ya mavazi
na vifaa vya masomo ambavyo vyote viliteketea kwa moto huo .
Bw
Mtove alisema mbali ya mkuu wa mkoa kutoa msaada huo wa bati na Madawati
wadau wengine waliofika kuchangia kituo hicho ni banki ya CRDB ambao
wamesaidia fotari kwa ajili ya kujengea kituo hicho.
Kwa
upande wake mkuu wa kituo hicho Padri Franco Soloberi alisema kuwa
wamepata faraja kubwa sana kutokana na jitihada mbali mbali
zinazoendelea kufanywa na serikali ya mkoa wa Iringa kwa kituo hicho
,kwani alisema mkuu huyo wa mkoa alikuwa ni mtu wa kwanza kufika
kusaidia kuzima moto na kusaidia msaada wa magodoro siku tukio hilo
lilipotokea .
Aidha
alisema msaada unaohitajika ni mkubwa kwani kituo hicho kinazaidia ya
watoto 50 ambao kwa sasa hawana sehemu ya kulala baada ya jengo hilo
kuungua moto.
EmoticonEmoticon