Msimamizi wa duka la Tigo la Ikwiriri Anthonia Nyalagwinda akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Juma Njwayo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya Tigo Ikwiriri wilayani Rufiji leo.
Ikwiriri,
Agosti 10 mwaka 2016- Wakazi
wa Ikwiriri mjini na vitongoji vya jirani sasa wanaweza kufurahia zaidi huduma
za Tigo, kutokana na uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la Tigo
lililofunguliwa leo katikati ya mji huo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka
hilo, Mkurugenzi wa Tigo wa kanda ya Pwani , Goodluck Charles alisema, ufunguzi
wa duka unaenda sambamba na mkakati wa kampuni wa kupanua na kuleta huduma zake
karibu na wananchi nchini kote.
“Hili ni duka sahihi kwa wateja kwa sababu linaleta
bidhaa na huduma zote za Tigo chini ya paa moja na kwa ukaribu zaidi. Pia liko
katikati ya mji ambapo linarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake
wanaotoka vitongoji vya mji wa Ikwiriri,
"alisema.
Duka hili jipya lililofunguliwa ni miongoni
mwa maduka mengine yaliyofunguliwa nchini, ambapo linajumuisha eneo ambalo
wateja watakaokuwa wanakuja kwa mara ya kwanza watafurahia kujifunza jinsi ya
kutumia bidhaa na huduma za Tigo kama vile matumizi ya simu za Smartphones,
modemu za intaneti na huduma nyingine za kimtandao kama vile Muziki wa Tigo na Facebook
ya bure inayotolewa na kampuni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kanda, duka
hili lililoko mtaa wa sokoni linatarajiwa
kuhudumia zaidi ya wateja 300 kwa siku, “idadi ambayo itapunguza usumbufu wa
kusafiri umbali mrefu ambao wateja wetu walikuwa wakiupata hapo awali katika
kutafuta huduma za Tigo kwenye maduka kama hili jijini Dar es Salaam”.
Akiongoza uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji
Juma Abdallah Njwayo alisema kwa kuleta huduma za Tigo karibu na wananchi, “duka hili jipya
litakuwa kichocheo katika kujenga fursa mpya za kiuchumi na kijamii kwa wakazi
wa eneo”.
Huduma za Mawasiliano kama zile zinazotolewa
na Tigo kama kupiga simu, ujumbe mfupi, kuunganisha intaneti, kufanya miamala
ya fedha kwa njia ya simu za mkononi na nyinginezo zimekuwa zikichochea
maendeleo ya kijamii na kiuchumi, alisema Njwayo huku akiwaasa wakazi wa mkoa
wa Pwani kutembelea duka hilo ili kujipatia huduma mbalimbali zilizosogezwa
karibu yao.
|
EmoticonEmoticon