Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya.
Suala la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.
Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.
Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.
Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.
Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.
Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
EmoticonEmoticon