Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu
cha wageni wakati alipotembelea ofisi za Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) leo hii kuona utendaji wa Baraza hilo.
Waziri
wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji
mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar
es Salaam kutokana utendaji usiolizisha.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Dionis Malinzi(kulia) akiongea jambo
na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye. Picha na Daudi Manongi.
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua
uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya
baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Mhe.
Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema
katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto
walizonazo.
“Baraza likirekebishwa vyama vya
michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika
michezo,”alisema Mhe. Nnauye.
Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba
ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna
mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu
alipoteuliwa mwaka 2009.
Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye
amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu
Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT
kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.
Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka
mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na
mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo
nchini.
Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu
Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya
kazi nyingine wizarani.
EmoticonEmoticon