Waziri Mkuu Kassim Majliwa
akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na
Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati
alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa
akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake)
kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Matishari matatu ambayo Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani
aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na
ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara
katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri
Mkuu)
………………………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari
ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry
Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo
kesho (Jumamosi) saa 6 mchana.
Waziri Mkuu
ambaye aliwasili Tanga leo mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy
Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua
kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani
kurejea Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo
fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka
apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo. Katika maswali
aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo
hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na
tugboat (meli ndogo).
“Nataka kesho saa
6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu
ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za
Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo
wa kujiendesha zenyewe (self propelled) “
“Nataka maelezo
ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi
hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya
Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za
kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi
wa fani hii?” alihoji Waziri Mkuu
“Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa,” aliongeza.
“Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa,” aliongeza.
Katika majibu
yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya
Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. “Pia wakati zinaagizwa
sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,” alisema Mkuu
huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es
Salaam.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa
Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na
kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari
ya magendo.
“Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu,
msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi
yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku
uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze
kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani,”
alisema Waziri Mkuu.
Alisema changamoto inayoikabili
Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani
ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.
Waziri Mkuu amerejea jijini leo jioni.
EmoticonEmoticon