Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akizungumza na Wabunge kutoka nchini Sweden (hawapo
pichani) leo jijini Da es salaam wakati wa mkutano uliofanyika Wizarani
hapo, kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden.
Kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof.
Mussa Assad.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya Serikali wakati wa mkutano na
Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya
kikazi nchini.
……………………………………………………………………………………………..
Waziriwa Fedha na Mipango,Mhe.
Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa Sweden katika ukumbi wa
Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina Tanzania na Sweden.
Katika mazungumzo yake na wabunge
hao ambao wamewasili nchini kwa ziara ya kikazi, Dkt. Mpango amesema
Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na inafanyakazi kwa ufanisi ili
kuhakikisha Watanzania wanapata huduma stahiki kutokana na rasilimali
zilizopo nchini.
Amesema Serikali imejipanga
kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kuiwezesha nchi
kujiendesha yenyewe na kuacha kutegemea misaada ya wahisani.
Aidha, amefafanua kuwa Tanzania
imejipanga kuongeza vyanzo vya ukusanyaji mapato pamoja na kuboresha
vyanzo vilivyopo na kuhakikishakila Mwananchi
anayestahilikulipakodistahikianalipa kwa wakati.
“Ni aibu kwa nchi yenye
rasilimali za kutosha Wananchi wake kuishi katika hali ya umasikini,
tunachotakiwa ni kuboresha kilimo kwa sababu wananchi wengi ndicho
wanachotegemea”, alisema.
Akizungumzia vipaumbele vya
Serikali katika mkutano huo, Dkt. Mpango alisema mkazo umewekwa zaidi
katika kufanya mapinduzi ya viwanda, ambapo nchi inaanzakuboresha
viwanda vilivyopo hususani vile ambavyo hutumia rasilimali
zinazopatikana nchini kama zile zinazotokana na kilimo.
Aliongeza kuwa katika kuboresha
viwanda pia Serikali ipo katika hatua za kuboresha soko la ndani na nje
ya nchi kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo.
Dkt. Mpango alisema sambamba na
kufanya mapinduzi ya viwanda, Tanzania imejipanga kuboresha miundombinu
ambapo mpaka sasa kuna miradi mbalimbali ya maendeleo imeanzishwa kama
mradi wa umeme vijijini.
Alisema katika suala la umeme,
nchi imeazimia kujikita katika uzalishaji wa kutumia vyanzo vingine kama
gesi asilia, jua na upepo kuliko kutegemea maji pekee.
Kuhusu sekta ya usafirishaji,
Dkt. Mpango amesema Serikali imejipanga kuboresha bandari zote nchini na
kuzifanya ziwe za kisasa ili kuhamasisha biashara za ndani na nje ya
nchi kupitia bandari hizo.
Hata hivyo, Dkt. Mpango alikiri
kuwa uboreshaji wa reli ya kati ni changamoto kwani reli hiyo haiwezi
kuboreshwa kwa kutumia fedha za bajeti ya Serikali pekee, hivyo Serikali
inajitahidi kutafuta njia za kufanikisha ujenzi huo.
Katika mkutano huo, Dkt. Mpango
alizungumzia suala la huduma za kijamii alisema, nchi imejipanga kutoa
elimu inayoendana na soko la ajira na Serikali imeanza kutoa elimu ya
msingi na sekondari bila malipo ili kuwawezesha wananchi wengi kupata
elimu.
Akizungumzia suala la uchumi,
Dkt. Mpango alisema hali ya uchumi kwa sasa ni nzuri kwani pato la ndani
la Taifa limefika asilimia 7 katika miaka ya hivi karibuni.
Dkt. Mpango alisema ili
kufanikisha vipaumbele hivyo, ni lazima maadili na nidhamu ya kazi
vifuatwe na watendaji pamoja na watumishi wa umma katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Aliongeza kuwa Serikali ipo
msatari wa mbele kupambana na rushwa na haitosita kuhakikisha watu wote
wanaohusika na rushwa wanachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande Wabunge kutoka nchini
Sweden, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Kenneth
Forslund, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada mbalimbali
zinazochukuliwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutoa huduma
za kijamii.
Tanzania na Swede nzime kuwa na
ushirikiano wa muda mrefu ambao umeifaidisha Tanzania katika shughuli
mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuendeleza miradi ya afya na umeme
hususani vijijini, elimu pamoja na kusaidia kukamilisha bajeti ya kila
mwaka.
Imetollewa na Msemaji
Wizara ya Fedhana Mipango
Kitengo cha Habari
19.2.2016
EmoticonEmoticon